JOYOUS CELEBRATION KUVUNJA REKODI TOLEO LA 20 MAANDALIZI YAANZA

Uwanja wa Moses Mabhida uliopo DurbanAfrika ya kusini

Maandalizi ya kurekodi DVD ya 20 ya kundi maarufu la muziki wa injili barani Africa la Joyous Celebration tayari yamekwisha anza kupitia vikao mbalimbali vinavyofanywa na kamati ya maandalizi ya kundi hilo huku mwaka huu kuna uwezekano mkubwa kundi hilo likarekodi DVD yake ya 20 katika uwanja wa mpira wa Moses Mabhida uliopo Durban mji ambao ndiko kundi hilo lilikoanzishwa.

Kamati hiyo ya maandalizi imeanza kutafuta sehemu ambayo wanadhani itafaa kwa kundi hilo kurekodi DVD yake ya 20 ambayo inatarajiwa kuwa ya aina yake,kamati hiyo imefika katika uwanja wa Moses Mabhida uliopo Durban nchini Afrika ya kusini mji ambao ndio unaongoza kwa kutoa waimbaji wengi wa kundi hilo wakiwemo viongozi wa kundi hilo na pia mashabiki wengi wa Joyous wanatokea mji huo.

Lindelani katikati akiwa katika uwanja wa Moses Mabhida na kamati ya maandalizi 

DVD hiyo inatarajiwa kurekodiwa mwezi December mwaka huu kama ilivyoada ya kundi hilo, ambapo kuna uwezekano mkubwa waimbaji wa toka kuanzishwa kwakundi hilo wakashirikishwa katika DVD hiyo ikiwa ni miaka zaidi ya 20 tangu kuanzishwa kwake. Aidha endapo kundi hilo litaamua kufanya rekodi hiyo katika uwanja wa mpira itakuwa imevunja rekodi yake na waimbaji wengi wa nchini humo ambao hawajawahi kurekodi katika viwanja vya mpira.

Wakati huohuo tayari kundi hilo limeachia kanda mpya ya sauti ama audio CD ya 19 toka juzi ambazo zimekwisha sambazwa madukani nchini humo huku pia ikianza kupatikana kwenye mitandao kama Spotify huku inatarajiwa kuanza kupatikana kesho katika mtandao wa  iTunes huku DVD inatarajiwa kuanza kupatikana mwezi ujao wakati wa uzinduzi wa toleo hilo ambalo walirekodi katika kitongoji cha Soweto mwezi December mwaka jana.

Kikao cha maandalizi kikifanyika
Hivi ndivyo lionekanavyo kava la toleo la 19 la Joyous Celebration


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.