KANSA YAKAMATA MWIMBAJI MWINGINE NYOTA, MAOMBI YAKO YANAHITAJIKAWapenzi wa muziki wa injili duniani na mashabiki wa kundi maarufu la Casting Crowns la nchini Marekani wameombwa kumuombea kiongozi wa kundi hilo Mark Hall ambaye amegundulika kuwa na uwezekano wa kansa katika moja ya figo yake hivyo inatakiwa kutolewa wiki hii.

Taarifa za Mark kugunduliwa na ugonjwa huo katika figo zilitolewa kupitia tovuti ya kundi hilo ambapo katika uchunguzi wa awali ilionekana anauvimbe mgumu katika figo yake ambapo aliporejea tena kwa uchunguzi madaktari wanauhakika wa asilimia 90 kwamba uvimbe huo ni kansa.

Nikiwa na Mark pamoja na Megan wa Casting Crowns baada ya kumaliza kuimba BCDO 2012 Uingereza.

Kutokana na majibu hayo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kuondoa figo moja iliyogunduliwa na ugonjwa huo siku ya jumatano wiki hii, na kuwataka watu waombe kwaajili ya afya yake ambapo amesema atakuwa sawa baada ya mwezi mmoja baada ya upasuaji au kwa muda mrefu zaidi ila amewataka watu kuombea afya yake na upasuaji unaotarajiwa kufanyika wiki hii.

Mark Hall ni baba wa familia ya watoto wanne na mke mmoja ambapo kundi lake la Casting Crowns linatamba na nyimbo mbalimbali ukiwemo wa 'Praise You In This storm'


Hey Casting Crowns Family,
I would appreciate your prayers.
Doctors found a solid mass in my right kidney about a week ago. They are 90% sure it's cancer and they are going to remove the entire kidney next Wednesday, March 11th. They believe the cancer is contained in the kidney, which is also a great hope. They will know more once it is out and Pathology can see it. 
I'll be in recovery for a month or a little longer because of the surgery. Please pray for healing and for God's peace for my family.
Praising Him in This Storm
Mark Hall
For updates please follow Mark Hall on Twitter at https://twitter.com/markhallcc and here on Facebook.
Mark akiwa na familia yake

Tazama 'Praise You In This storm' live 


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.