KUELEKEA TAMASHA LA PASAKA TAR 5 APRILI, TUJIKUMBUSHE


Kati ya kumbukumbu ambazo bado ziko dhahiri kichwani mwangu ni ile huduma ambayo Pastor Solly aliifanya uwanja wa taifa kwenye tamasha la Krismasi mwaka 2013. Solly akiambatana na waimbaji wake kutoka Afrika Kusini, aliwashangaza watu kwa namna alivyojaa kwenye jukwaa, yeye mwenyewe akiwa ushuhuda wa kutosha kutokana na maisha yake, hadi kufikia hapo alipo. Kama hujui ni kwamba Solly Mahlangu alizaliwa baada ya mama yake kubakwa, na hajawahi kumfahamu baba yake tokea azaliwe. Bofya hapa kusoma habari hiyo.

Kwanza tazama video tatu mfululizo ambavyo Mchungaji Solly Mahlangu alihudumu mnamo 2013.


Alivyoanza


Pokea Sifa/Mwamba Mwamba


One Love

2014 imepita, na sasa ni 2015 na tamasha la Pasaka linawadia. Hapa tunaongelea miaka 15 tokea kuanzishwa kwa matamasha haya chini ya kampuni ya Msama Promotions. Tayari kwa Kiswahili chake hafifu Mchungaji Solly ambaye ni dhahiri anapakumbuka Uwanja wa Taifa amekiri kuwepo kwenye tukio hilo kubwa na la kihistoria, ambapo kwa wakati huu kutoka Afrika Kusini hatokuwepo peke yake, bali pia na Malkia wa muziki wa injili barani Afrika, Bi Rebecca Malope. Kama hukumuona Malope kipindi akiwa Tanzania basi unaweza kubofya hapa.

One Love - Rebecca Malope
 

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.