KWA TAARIFA YAKO HUYU NI MMOJA KATI YA WAIMBAJI WA SASA WA JOYOUS INAYOJIFUNIA

Mashambulizi Joyous 19
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
KWA TAARIFA YAKO hii leo tupo nchini Afrika ya kusini ambako tutakujulisha kuhusu mwimbaji mpya wa Joyous Celebration ambaye anazungumzwa sana midomoni mwa mashabiki wa kundi hilo nchini humo na nje ya nchi hiyo ambao wamesikiliza kazi za kundi hilo kuanzia toleo la 17 mpaka toleo jipya la 19 ambalo DVD pamoja na CD tayari zimeshaanza kuuzwa na kuvunja rekodi ya mauzo nchini humo ndani ya wiki moja tangu kuanza kuuzwa.

KWA TAARIFA YAKO mwimbaji tunayekufahamisha hii leo japo kwa ufupi ni mwanakaka Sibusiso Desmond Noah Mthembu, mwimbaji huyu amebarikiwa sauti inayowabariki wengi. Katika DVD mpya ameshiriki kuimba kama mwanzishaji katika nyimbo tatu ukiwemo wimbo maalumu kwaajili ya mwimbaji wa kundi hilo aliyefariki mwezi Disemba mwaka jana Lihle Mbanjwa, uitwao Haleluyah Nkateko huku DVD ya 18 akiimba pambio lililomuongezea umaarufu la Umoya praise medley lakini safari yake aliianza rasmi katika DVD ya 17 akiimba wimbo wa kitamaduni.

KWA TAARIFA YAKO kabla mwimbaji huyu hajajiunga na Joyous, alibahatika kuonwa na mmoja
wa viongozi wa Joyous bwana Lindelani Mkhize (choirmaster) akiimba nyimbo kanisani ambapo kiongozi huyo akamfuata kijana huyo na kumwambia aende akajiunge na Joyous, mwaliko ambao aliufurahia lakini alimuomba kiongozi huyo kumvumilia mpaka amalize shule ndio aje kujiunga jambo ambalo alikubaliwa na kweli alipomaliza shule alikaribishwa moja kwa moja kundini humo.


KWA TAARIFA YAKO kijana huyu ambaye huwa anamshukuru Mungu kila iitwapo leo kutokana na nafasi aliyompa ya utumishi, kwani akiangalia alikotoka hakuwa na kitu, nguo pia alikuwa nayo moja kauka nikuvae lakini sasa anauwezo wa kubadili na kabati lake linaonyesha kuna nguo, ameongeza kuwa katika familia yao ni yeye pekee ambaye ameonekana kupewa akili zaidi na neema ya kufika chuo kikuu, lakini pia aliweka wazi kwamba hana kumbukumbu yeyote aliyoachiwa na baba yake ambaye alifariki wakati mwimbaji huyo mdogo na kuwaambia mashabiki wake katika ukurasa wake wa Facebook kwamba picha aliyokuwa ameweka anafanana kabisa na baba yake, hivyo sura yake anamwakilisha marehemu baba yake.KWA TAARIFA YAKO aidha kuna siku Sibu aliweka wazi kwenye ukurasa wake wa facebook akiwashukuru watu waliokuwa wakimtukana kupitia inbox lakini pia aliwashukuru wale wote wanaomtia moyo, na kumpongeza kwa kazi nzuri ndani ya Joyous Celebration. Aidha Noaha alianza kuaminika toka mwanzoni alipojiunga kwani alipewa wimbo kuanzisha kwenye tamasha la Joyous Rewind, walipoenda Ghana mwimbaji huyo alipewa aanzishe pambio la Phindukhulume, lakini pia watu wengi wakiwemo viongozi wa Joyous na waimbaji wa kundi hilo wamemtabiria kijana huyo kufanya makubwa sana kwenye medani ya uimbaji.

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO wiki ijayo... hii leo, vinginevyo tukutane wiki ijayo...
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.