KWA TAARIFA YAKO: MOJA KATI YA WACHUNGAJI WALIOBARIKIWA NA HUDUMA ZA WATOTO WAO

Mchungaji kiongozi wa Hillsong Brian akiwa pamoja na mtoto wake wa kwanza na mkewe siku walipoagwa kuelekea Marekani kusimamia tawi la kanisa hilo mjini LA.
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

KWA TAARIFA YAKO hii leo tunakutaarifu jambo kutoka nje ya bara la Afrika, kumekuwa na kasumba ama taarifa nyingi zikisema kwamba kati ya familia ambazo wazazi hupata shida katika kuwalea watoto wao ili waende sawa kwa kufuatisha kile wanachowafundisha na badala yake watoto wamekuwa wakifuata kitu kingine basi ni familia za wachungaji na viongozi wa dini, mara nyingi taarifa zinasema watoto wao hufanya mambo tofauti na yale wafundishayo wazazi wao kwa mfano, baba mchungaji lakini mtoto licha ya kubarikiwa kipaji cha uimbaji basi atakwenda kuimba mziki wa nje ya kanisani au kuwa na marafiki wa aina ambayo huleta mushkeli kwa watu kuamini kwamba mtoto wa mchungaji anaweza kufanya hivyo.


Brian na Bobbie Houston wasimamizi wakuu wa kanisa la Hillsong
KWA TAARIFA YAKO basi hii leo tunataka kukufahamisha moja ya familia ambazo hapana shaka wazazi wanafurahi ama wanaamani kuona watoto wao wanafuata nyendo zao. Familia hiyo si nyingine bali ni familia ya mwanzilishi na msimamizi wa kanisa maarufu duniani la Hillsong lenye makazi yake nchini Australia mchungaji Brian na Bobbie Houston ambao kwa pamoja Mungu amewabariki watoto watatu Benjamin, Joel pamoja na Laura ambao wote kwa pamoja wameshaanzisha familia zao kwasasa.

KWA TAARIFA YAKO watoto wa mchungaji huyu wamekuwa msaada sana kwa kanisa la Hillsong, ukianza na mkubwa aitwaye Benjamin au Ben Houston pamoja na mkewe Lucille ambao kwasasa anaishi Los Angeles nchini Marekani, ni mchungaji kiongozi wa kanisa hilo huko LA ambako kanisa hilo lilifungua tawi mwanzoni mwa mwaka jana 2014 ingawa awali alikuwa akitumika katika kanisa hilo nchini Australia.


Joel na familia yake

KWA TAARIFA YAKO mtoto wa pili wa mchungaji huyu ambaye ni maarufu zaidi kuliko ndugu zake ni Joel Houston ambaye yeye amejikita kwenye uimbaji, ni mmoja wa watunzi wa kutumainiwa wa Hillsong ameshiriki kutunga kati ya nyimbo maarufu za kundi hilo ukiwemo, The Stand, from the inside out, love is war, relentless, Oceans, Scandal of Grace, Aftermath, Glorious ruins na nyingine nyingi. Kwasasa amejikita zaidi kwenye kundi la Hillsong United ingawa pia anapatikana kwenyeb kundi mama la Hillsong Worship. Joel pamoja na mkewe Zoe na mtoto wao nao wanaishi New York nchini Marekani ambako kanisa hilo limefungua tawi lake huku Joel akiwa kiongozi wa sifa.
KWA TAARIFA YAKO kitinda mimba wa familia hii ambaye ni binti wa pekee Laura Houston au mwite Mrs Toggs  yeye yupo Australia ambako anaishi na mumewe pamoja na mtoto wake, ila pia kwa cheo yeye ni na mumewe ni wachungaji wa vijana wakisimamia kundi jipya la muziki la Hillsong Young and Free (Y&F) ambao tayari wameshatoa album mbili mpaka sasa


Binti wa pekee katika familia hiyo, mchungaji Laura Toggs

Tazama Hillsong Young and Free toleo lao la kwanza walilomshirikisha Taya Smith wa H.United

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa leo, vinginevyo jiunge nasi wiki ijayo…
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.