KWA TAARIFA YAKO: SAFARI YA ANGEL KABLA YA KUMGEUKIA MUNGU

Angel Benard
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

KWA TAARIFA YAKO hii leo tupo kukujulisha kama hufahamu kuhusiana na mama ambaye amebarikiwa na Mungu linapokuja suala la uimbaji na namna alivyoweza kuwabariki watu wengi toka aanze uimbaji wa muziki wa injili ila pia watu hawafahamu kwamba kabla ya kuwa mwimbaji wa muziki wa injili kuna yapi aliyopitia katika muziki. KWA TAARIFA YAKO mwimbaji tunayetaka kukufahamisha si mwingine bali ni mwanadada Angel Benard ambaye kwasasa anatamba na album yake mpya iitwayo 'Need You To Reign'.

KWA TAARIFA YAKO kama hufahamu Angel amebarikiwa sauti toka zamani na kwamba kabla ya kuokoka alishawahi kushirikishwa kwenye kazi za muziki wa dunia, moja ya kazi aliyoshirikishwa ilikuwa wimbo uitwao 'Sema' na mwanamuziki Pig Black ukiacha wengine ambao walikuwa wakiomba kumshirikisha bila mafanikio. KWA TAARIFA YAKO ili kuonyesha kwamba aliitwa kwenye huduma ya kumtumikia Mungu  Angel alikuwa mbioni kutoa album yake ya muziki wa dunia ambayo alifanikiwa kuirekodi yote katika studio za "Serious Records" huku akiwa amewashirikisha waimbaji kama Nuruelly, Dullayo pamoja na Pig Black mwaka 2009 


Tazama wimbo "Need You To Reign" uliobeba album mpya ya Angel 


KWA TAARIFA YAKO kama hufahamu Angel amesema lakini kabla hajaitoa rasmi album hiyo, bila kufuata mkumbo anasema alimkabidhi Yesu maisha yake alipokuwa kanisani E.A.G.T Mito ya Baraka kwa Askofu Bruno Mwakibolwa cha ajabu hajajua kilichotokea ila album yake na waimbaji wengine zilifutika studio siku mbili baada ya kuokoka, kitu ambacho yawezekana Mungu pia hakutaka mwimbaji huyu kuwa na kumbukumbu ya album ya muziki wa nje ya kanisa. Ya Mungu mengi. KWA TAARIFA YAKO nyota ya Angel iliweza kung'aa zaidi na jina lake kufahamika zaidi pale alipojiunga na kundi la Glorious Celebration ambako aliweza kuongoza vyema wimbo wa 'Niguse, Ee Roho na nyinginezo kabla ya kutoka huko na kusimama peke yake kama mwimbaji wa kujitegemea.

KWA TAARIFA YAKO uimbaji wa Angel unabariki wengi na si ajabu hata pale malkia wa muziki wa injili barani Afrika mwanamama Rebecca Malope kushindwa kujizuia pale alipomsikia Angel Bernard anaimba na Glorious kwenye tamasha la pasaka uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam mwaka juzi. Angel anataka kupanua zaidi huduma yake kwa kuwagusa waliopondeka moyo na wale ambao hawajamjua Kristo ili wakapate kumjua na kumkubali kuwa BWANA na Mwokozi wa maisha yao. Kwa kuonyesha hilo album yake mpya imechanganyika nyimbo za kiswahili na kiingereza na tayari nyimbo mbalimbali zimeonyesha kupokelewa vyema na wapenzi wa muziki wa injili nchini.

Tazama Angel na Glorious Worship Team uwanja wa Taifa Rebecca Malope akifurahia uimbaji wao

Pata ujumbe kupitia wimbo huu
Timu inayohudumu pamoja na Angel mara baada ya kupatikana jijini Arusha.


Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO hii leo, vinginevyo tukutane wiki ijayo…
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.