KWETU PAZURI WAACHIA WIMBO MPYA HII LEO, KUENDELEA KUSHIKILIA CHATI KAMA KAWAIDAHaya hii ni habari njema kwa wapenzi wa kundi la Ambassadors of Christ Choir kutoka Remera SDA Kigali Rwanda. Hii leo wameachia wimbo mmoja ambao utakuwemo kwenye DVD yao mpya inayotarajiwa kutolewa rasmi mwezi ujao. wimbo unaitwa 'Siku za kilio zimepita'.

Ambapo kwa mujibu wa video fupi ya utangulizi inayopatikana kwenye mtandao wa Youtube, wimbo huu ni maalumu kuonyesha kwamba kwaya hiyo imesimama imara tena katika kumtangaza Kristo licha ya ajali mbaya waliyoipata mwaka 2011 wakitokea Tanzania ambapo wenzao watatu walipoteza maisha huku wengine watatu wakijeruhiwa vibaya ambao pia wanaonekana katika video hii mpya kwamba wanaendelea vyema na maisha yao na familia zao hakuna kilio tena.

Wimbo huu utafanyika baraka tena kwa wapenzi wa kwaya hii, kutokana na ujumbe mzuri uliomo, sauti bila kusahau mziki mzuri pamoja na video ya kupendeza iliyochanganywa na picha mbalimbali za kundi hilo wakiwa kwenye huduma nchini Zambia na kwao Rwanda. Kubwa zaidi mwalimu wao bwana Ssozi ndiye aliyeanzisha wimbo huo.Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.