LICHA YA HOLLYWOOD KUTOMTAKA KUMZUNGUMZIA YESU, BADO AENDELEA KUSHUHUDIA

Denzel Washington
Mkongwe na nyota wa filamu duniani Denzel Washington ameonekana kwenda kinyume na kundi la wasioamini na wapinzani wa dini huko Hollywood nchini Marekani kutokana na tabia yake ya kuzungumza juu ya imani yake kama Mkristo.

"Ninasoma Biblia kila siku, pia ninasoma neno la kila siku" alikaririwa mkongwe huyo alipozungumza na GQ. Baba yake alikuwa mchungaji wa kanisa la Pentekoste nayeye amelelewa na kukulia kwenye nyumba ambayo Mungu alifanyika namba moja kwakila jambo."Alikuwa na kanisa lake, na ilikuwa jumapili inakuwa ndefu kwakuwa inakubidi uwe kanisani siku nzima" alisema Washington

"Watu nilioishi nao hawakuwa na baba mimi nilikuwa na baba, baba yangu alikuwa mtu mwema, alikuwa mtu wa kiroho sana na mwenye muonekano mzuri" aliongezea Washington. Kuwa na mwanaume wa aina ya baba yake kumempa upendeleo Washington, kwakuwa mpaka sasa bado ameendelea kusimamia alichofundishwa licha ya umaarufu na utajiri alioupata katika maisha yake.

Mwigizaji huyo ameomba wasomaji wa habari hii kama alivyohojiwa kwamba wakumbuke kuanza siku yao kwa maombi kabla ya kuelekea kwenye shughuli zao za kila siku.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.