MAMBO MACHACHE AMBAYO HUPASWI KUSAHAU MAISHANI MWAKO

Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.

Familia Yako.
Kila mtu unayemuona leo ni matokeo ya familia. Hakuna mtu ambaye hakutokeo kwenye mfumo wa Familia. Familia ndio msingi bora kwenye kila jamii ya watu. Ukitaka kujua aina ya jamii na aina ya taifa ambalo watu wake wanaishi, hakikisha unaangalia mifumo ya uendeshaji katika taifa hilo. Taifa lolote ambalo lina mfumo finyu wa kujua umuhimu wa familia na kutokufanya familia kama moja ya vipaumbele, mara nyingi maendeleo yake huwa duni. Maendeleo yoyote unayoyaona leo duniani yalianzia kwenye familia. Hakuna jambo liliwahi kuzuka zuka tu hewani kama halikuanzia kwenye familia. Hakikisha katika kila unachofanya familia yako inakuwa kipaumbele kwenye kila hatua. Maamuzi yoyote unayoyafanya hakikisha unajumuisha familia yako.
©appeal for purity

Jinsi Yako.
Kwenye dunia ya leo tumekuwa na mkanganyiko mkubwa sana sababu tumeshindwa kutofautisha kati ya jinsia tulizo nazo na majukumu tulio nayo. Hiki ndio kizazi ambacho mwanaume anatamani kuwa mwanamke na mwanamke anatamani kuwa mwanaume. Unapoweza kutambua na kuelewa jinsia uliyo nayo kikamilifu itakusaidia kujua aina ya majukumu ulio nayo kwenye jamii. Miaka ya nyuma majukumu ndio yalikuwa yanaweza kutofautisha jinsia, lakini leo haiko hivyo. Kama kazi aina fulani jinsi zote zina uwezo wa kufanya. Ni Muhimu kujua na kutambua wajibu wako iwapo ni mwanamke/mwanaume na uelewe kitu gani unapaswa kufanya kwenye maisha yako.Hakikisha kama mwanaume unajitambua, na kama ni mwanamke unapaswa kujitambua kama mwanamke na unaweza kutambua na kutofautisha aina ya majukumu ulio nayo lakini pia unatambua utofauti uliopo kati ya jinsi moja na nyingine kwenye maisha ya kila siku.


Mfumo wa Maamuzi Yako.
©mac
Kila mmoja ana namna ya kufanya maamuzi yake. Kila mmoja ana filosofia yake ya namna ya kufikiri na namna ya kufanya maamuzi.Maamuzi ya kila mtu ni aina ya BLUE PRINT ambayo inaweza kutofautisha kati ya mtu mmoja na mwingine. Unaweza kukuta mtu fulani kwenye maamuzi fulani anapata taabu sana lakini kwa mwingine ni kawaida sana na ni rahisi. Unapoona mtu umeshindwa kwenye jambo fulani kwenye maisha inakupasa kurejea aina ya filosofia unayotumia kufanya maamuzi yako ya kila siku. Hakuna kushindwa kwenye jambo lolote kama mfumo na filosofia haukuwa mbovu. Tathmini mara kwa mara mfumo wako wa maamuzi. Ukiona mfumo wako wa maamuzi unakuletea matokeo bora kila siku endelea nao na ukiona unakufanya ushindwe, ubadilishe. Maana mfumo wako wa maamuzi ndio BLUE PRINT yako unaokutofautisha kati yako na mwingine.

Kanuni za Maisha.
Tunapoona leo kuna Uhai kwenye sayari iitwayo dunia kwa miaka mingi iliyopita ni dhahiri kuna kanuni na mifumo inayoongoza maisha ya kila siku ndio maana kuna uhai. Kanuni na taratibu za maisha hubadilika kulingana na uhitaji wa jamii husika. Kwenye maisha kuna vitu unapaswa kufanya na vingine haupaswi kufanya (Do’s and Don’ts). Iwapo kwenye mfumo wa maisha umeambiwa hiki hakipaswi kufanywa, acha usifanye. Iwapo umeambiwa hiki kinapaswa kufanyika, imekupasa kufanya. Kwa kizazi chetu siku zetu za Uhai zimekuwa fupi sababu hatutaki kufuata kanuni na taratibu za msingi za maisha na uhai. Ukiambiwa fuata sheria na taratibu za kula ili usiuguwe magonjwa wewe fanya maana ni kwa faida yako. Umeambiwa usitumie vilevi fulani, acha usitumie. Ni ngumu kuendelea na Uhai kwenye maisha wakati hatufuati kanuni za msingi za Uhai na Maisha. Umeshawahi kujiuliza kanuni ya Uhai ingekuwa kila mtu anapaswa kumuua mwingine ili uhai uendelee unafikiri nini kingeendelea? Au kila mtu anapaswa kunywa sumu ili afe mwingine aishi unafikiri nini kingeendelea? Je, Uhai na maisha tulio nayo yangekuwa hapa tulipo?

Hitimisho.
Kuna mambo mengi ambayo hatupaswi kuyasahau kwenye siku za Uhai wetu na maisha yetu ya kila siku. Lakini wewe ni shahidi namna tunavyojisahaulisha, madhara yake yanaweza yasiwe moja kwa moja lakini baada ya muda fulani madahara huanza kujitokeza na kuathiri maisha yetu na uhai wetu kama wanadamu. Nimezungumza mambo machache lakini yapo mengi hakikisha huyasahau mambo Muhimu ambayo yanaweza kukufanya uendelee kuishi. Jenga na wekeza muda wa kuyaendeleza. E-mail:naki1419@gmail.com +255788454585 God Bless Y’All
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.