MCHUNGAJI AWAKODIA CHANGUDOA HOTELI YA KUPUMZIKIA NA KUWAPA INJILI ASUBUHI YAKE

Mchungaji Simon kushoto pamoja na mmoja wa wenyeji wake nchini Burundi anakofanya huduma yake.
Katika kuhakikisha anapeleka injili kusikofikirika, mchungaji Simon Guillebaud mzaliwa wa Sussex nchini Uingereza akifanya kazi ya injili nchini Burundi, alimua kupeleka injili kwa wadada wanaojihusisha na biashara ya kuuza miili yao nchini Burundi kwakuwakodia hoteli ya kupumzika usiku kucha na kuwahubiria siku iliyofuatia.

Mchungaji huyo ambaye ni mwanzilishi wa huduma ya Great Lakes Outreach aliamua kumshirikisha rafiki yake anayemuamini ili kufanikisha kuwapata wadada hao ili kuzuia taarifa mbaya endapo angeonekana yeye binafsi akiwafatilia wadada hao. rafiki yake alifanikiwa kukutana na wadada hao waliotambuliwa kwa majina ya Arlette (22) pamoja na Divine (21).

Rafiki wa mchungaji huyo alifanikiwa kuwapata wadada hao na kuwafikisha hotelini ambako mchungaji huyo aliwaambia amewakodi ili wadada hao walale hotelini hapo na kula chochote wanachokipenda usiku mzima bila kuwabughudhi wapangaji wengine hotelini na kwamba gharama zao atalipa yeye asubuhi atakaporejea hotelini hapo.

Kwa mujibu wa mchungaji Guillebaud amesema asubuhi yake alipokutana nao walionekana kuaminika zaidi, anasema aliwaza kwamba mabinti wadogo hawana ndoto kwamba watakapokuwa wakubwa wanataka kuwa changudoa lakini wakati mwingine mambo ya ajabu hutokea maishani na kukupeleka katika uamuzi mbaya lakini pia mambo yanaweza kubadilika kama wanataka alisema Guillebaud.

Mchungaji huyo ameandika kwenye blog yake kwamba amejifunza kwamba mabinti hao walijiingiza katika uchangudoa ili kujisaidia wao na familia zao kwakuwa walikuwa yatima pesa walizopata walizitumia kulipa kodi na ada ya shule." Niliwauliza ndoto zao ni zipi, walijibu wanataka kufanya biashara ndogo ndogo au kuwa wafanyabiashara kitu ambacho kilinifikirisha kwamba kama wamefanya uamuzi mzuri kuanzia leo je baada ya miaka 10 nani ajuaye watakuwa wanaendesha biashara kubwa, wanaishi maisha ya furaha na waume na watoto wao?

Mchungaji Simon na familia yake.
Baada ya kuongea nao asubuhi hiyo mchungaji Guillebaud alipanga kukutana tena na wadada hao kwaajili ya ushauri wa maisha yao ikiwa pamoja na kuwakaribisha kanisani. Alipokutana nao tena walikubaliana wamalize kwanza shule kwa muhula uliobakia kabla hawajaanza biashara na kwamba waliweza kupanga bajeti ya biashara waliyotaka kuifanya ili kuondokana na matatizo ya wanachokifanya kitendo ambacho mmoja wao kilimfanya acheke na kusema wamepata tumaini hawatarudi tena kufanya biashara ya kuuza miili yao.

Mchungaji Guillebaud amesema anatumaini kukutana na wanawake wengi zaidi wanaouza miili yao ili kuondokana na shughuli hiyo " Nina ndoto ya kuwa mfano kwa wengine tukifanya hivi kwa miaka mingine ijayo bila kuacha ili kubadili historia ya wadada wengine na kuwaonyesha kwamba wanaweza kuanza maisha yao kwa upya kwakuwa uwezekano huo upo kwakuwa hawajasahaulika, kutopendwa au kuachwa" alisema mchungaji Guillebaud

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.