MCHUNGAJI KATIKA MATATIZO BAADA YA KURUHUSU WAISLAMU KUFANYIA IBADA YAO KANISANI

Kanisa la Kianglikana la Mtakatifu John, Waterloo jijini London©telegraph
Mchungaji kiongozi wa kanisa la Kianglikana la mtakatifu John lililopo katikati ya jiji la London maeneo ya Waterloo, Canon Giles Goddard amejikuta katika wakati mgumu kutoka kwa wahubiri wenzake pamoja na baadhi ya Wakristo baada ya kuwakaribisha waumini wa dini ya kiislamu kufanya ibada yao katika kanisa hilo.

Kwa mujibu wa gazeti la Telegraph la nchini Uingereza limeripoti kwamba mchungaji huyo aliwataka waumini wake kumshukuru "Mungu kwamba wanampenda Allah" huku akisema ibada hiyo ya waislamu ambayo pia alikaribishwa na kusoma kifungu kutoka kwenye Biblia ilikuwa ya aina yake hasa kutokana na kuwapa waislamu sehemu ya kufanyia sala yao baada ya waumini wa dini hiyo kumuomba nayeye bila hiana aliwakaribisha bila kujua kuwa ingeleta mkanganyiko kutoka kwa wenzake.

Baadhi ya wainjilisti walionyesha hasira yao wakidai ibada hiyo ilikuwa kinyume cha sheria kwakuwa
Mchungaji Goddard siku ya majivu 
sheria ya kanisa hilo hairuhusu ibada yeyote ambayo ni kinyume na kanuni za kanisa la England yaani Anglikana (Church of England). Aidha mchungaji Goddard amekaririwa akisema "tunatoa nafasi kwa watu kufanya ibada kwahiyo na ndivyo alivyofanya kwahiyo hajavunja sheria za kanisa" aliliambia gazeti hilo. labda wangeenda kwenye ukumbi wa halmashauri,lakini wamependa kufanyia kanisani, na walifurahia na kupendezewa kwakukaribishwa na ilikuwa ya aina yake kwakuwa ni Mungu mmoja" alisema mchungaji Goddard.

Kwa upande wake mchungaji Stephen Kuhrt wa kanisa la Christ Church, New Malden kusini magharibi mwa jiji la London ameliambia gazeti hilo kuwa hajapendezwa na hatua aliyochukua mchungaji mwenzake kuruhusu waislamu kufanyia ibada kanisani kwake nayeye pia kushiriki katika ibada hiyo, kwakuwa hiyo haitawezekana kwa wakristo kukaribishwa msikitini kuendesha ibada yao na kwamba alichofanya mchungaji mwenzake ni kosa.

Waumini wa kiislamu wakifanyiwa mahojiano kanisani humo na kituo cha Itv cha nchini Uingereza


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.