RAIS MKAPA, KADINALI PENGO WAALIKWA TAMASHA LA PASAKA


Na Mwandishi Wetu

RAIS wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa ni mmoja wa waalikwa wa Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama Mkapa ni kiongozi wa kitaifa ambaye anastahili kuhudhuria tamasha hilo ambalo linatimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake.

Msama alisema sambamba na Mkapa, wamemwalika Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Muadhama Polycalp Kadinali Pengo kwa lengo la kufikisha neno la Mungu kwa binaadam wote kwa sababu linashirikisha waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania.

Msama alisema wanaendelea kuwasilisha mialiko mbalimbali kwa viongozi wakiwemo wabunge, marais na viongozi wa dini.

“Tunahitaji maneno matakatifu ya viongozi wa dini na serikali kwa lengo la kumlilia Mungu kwa matukio yanayotokea hapa nchini,” alisema Msama.


Wakati huohuo muimbaji chipukizi wa muziki wa injili Tanzania, Christopher Mwahangila ametabanaisha kuwasilisha albamu yake ya ‘Mungu ni Mungu tu’ ikiwa ni mara ya kwanza kushiriki tamasha la Kimataifa la Pasaka linalotarajia kufanyika mwezi ujao kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwahangila albamu hiyo ya tatu tangu kuanza kuimba ina nyimbo saba ambazo ni ‘Huruma ya Mungu’, ‘Hudumia kusanyiko’, ‘Unamuhitaji Yesu’,‘Mipango ya ibilisi imegoma’, ‘Nimekubali’ na ‘Ametenda Maajabu’ ataiwasilisha albamu hiyo kwa Watanzania na wageni watakaohudhuria tamasha hilo.

Mwahangila alisema ushiriki wake katika tamasha hilo ni ndoto aliyowahi kuota miaka kadhaa iliyopita kwamba anataka kushiriki matamasha ya kimataifa.

Aidha Mwahangila alitoa wito kwa waumini kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ili kupata neno la Mungu kutoka waimbaji wa Kimataifa.

“Tamasha la Pasaka limebeba watumishi ambao Mungu amewatumia kwa viwango vya juu,” alisema Mwahangila.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.