NINAWEZA KUIMBA: KUMI BORA WALIOFUZU HATUA YA MWISHO

Kwa wale wote waliopata kushiriki msimu wa kwanza wa shindano la Ninaweza Kuimba, hatimaye mchujo uliopo umefikia watu kumi, ambapo kati ya hao, ni watu watano tu watawakilisha.

Kiujumla, haikuwa kazi rahisi katika kufikia haya majina kumi, watu wengi wana viwango kiasi kwamba tungeweza kupata hata watu ishirini wa kuingia studio na kurekodiwa video bure, kama isingekuwa kwa vigezo na masharti ya shindano hili kwa msimu huu wa kwanza. Kama kutakuwa na fursa yoyote, kulingana na sauti zilizotumwa, hatutosia kuwasiliana na yeyote yule - iwe amefika kumi bora ama hata kama hakufika.

Kwa hivi sasa, waliofuzu hadi kufikia hatua hii ya mwisho ni wafuatao, katika mpangilio wa herufi.
  1.  Aron Suluba - DSM
  2.  Dorcas Samuel- DSM
  3.  Esther Peter - DSM
  4.  Faraja Mbijima - DSM
  5.  Glorysima Venant - DSM
  6.  Grace Tenga - DSM
  7.  Janson Jackson - DSM
  8.  Sophia Mbaga - DSM
  9.  Victor Ngosso - Arusha
  10.  Yusuph Nahshon - Arusha
Hatua inayofuata ni kuchuja hadi kufikia watu watano tu, kwa walio Dar es Salaam - mawasiliano yatafanyika ili kupewa maelekezo zaidi. Halikadhalika kwa walioko Arusha maelekezo yatatolewa pia. Iwapo kuna swali la aina lolote ile kutoka kwa washiriki, tafadhali msisite kutuandikia ujumbe mfupi wa maandishi kupitia 0713554153 ama kwa barua pepe, uimbaji@inhouse.co.tz

Tunashukuru sana kwa walioshiriki, na tunawatakia kila la heri kwenye huduma yao, kama hukufanikiwa kwa msimu huu, basi una fursa ya kujipanga kwa ajili ya msimu ujao. Usijisikie vibaya.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.