PASTOR SOLLY MAHLANGU AWASHA MOTO JIJINI LONDONMwimbaji nyota wa Afrika ya Kusini, mchungaji Solly Mahlangu ambaye yupo nchini Uingereza kwa ziara ya uimbaji, usiku wa kuamkia leo aliwasha moto wa injili jijini London katika ukumbi wa Castle Green, Essex uliojaza mamia ya wakazi wa jiji hilo na vitongoji vyake ambao kwa pamoja mwanzo mpaka mwisho wa onyesho hilo walionekana kuguswa na huduma ya uimbaji ya mwimbaji huyo.

Katika onyesho hilo mchungaji aliimba nyimbo zake zote maarufu kutoka katika album yake ya kwanza mpaka ya sasa, ambapo umati wa watu waliohudhuria tamasha hilo wanatokea Zimbabwe, Afrika ya kusini na wachache kutoka Afrika magharibi ambao kwasasa makazi yao ni nchini Uingereza. Mwimbaji huyo aliyewahi kufika Tanzania, anatarajiwa kuendelea na ziara yake hapo kesho kwakufanya tamasha jijini Glasgow nchini Scotland

Mambo yalipendeza katika tamasha hilo kama picha zinavyoonyesha©Unc Charles 


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.