RAIS KIKWETE ATEUA WABUNGE WAPYA WAWILI BUNGE LA JAMHURI

Ikulu ya Magogoni. ©TheHabari
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wabunge wawili (2) wapya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Walioteuliwa ni Dkt. Grace Khwaya Puja na Bwana Innocent Sebba.

Rais amefanya uteuzi huu  kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 66 (I) (e) ambapo amepewa mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi 10.

Uteuzi huu umekamilisha idadi ya wabunge ambao Mheshimiwa Rais amepewa  kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo Kikatiba.

Wabunge ambao wameshateuliwa ni:
-       Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
-       Mhe. Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo
-       Mhe. Dkt. Asha Rose Migiro
-       Mhe. Janet Zebedayo Mbene
-       Mhe. Saada Salum Mkuya
-       Mhe. Zakhia Hamdani Meghji
-       Mhe. Shamsi Vuai Nahodha
-       Mhe. James Fransis Mbatia

Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Machi,

Taarifa ya Ikulu.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.