SIKU NNE KABLA YA UZINDUZI MWIMBAJI JOYOUS CELEBRATION ATANGAZA KUNG'ATUKAZikiwa zimebaki siku nne kabla ya kundi la Joyous Celebration kuzindua rasmi CD na DVD yake ya 19, mwimbaji nyota wa nyimbo za kitamaduni wa kundi hilo mwanadada Sphumelee Mbambo ama Ntokozo kwa jina lake lingine, ametangaza kuondoka katika kundi hilo baada ya safari yake ya miaka saba tangu ajiunge na kundi hilo.

Sphumelele ameweka wazi kuhusu uamuzi wake huo na kusema kwamba amepata baraka zote kutoka kwa viongozi wa kundi hilo na pia amewashukuru kwa kumpa nafasi ya kuwemo kundini na kujifunza mengi ambayo yamemfanya kukua kiuimbaji na kiroho. Mwimbaji huyo amewashukuru mashabiki na wote waliomuunga mkono kwa wakati wote bila kusahau watu ambao bado hawamuelewi mwimbaji huyo huku yeye pia akisema hata yeye huwa hajielewi lakini Mungu anamtumia vile apendavyo kwa utukufu wake. Soma ujumbe wake hapo chini kama alivyouweka jana usiku.


    News Feed

    From day one ngifika kuMusic industry nangamukela ngothando nangi votela on I want to sing Gospel ngaphuma position 5 ngabizwa kwi Joyous Celebration for 7years uThixo uhambe nami ngibonga uThixo owasebenzisa uKhabazela, uJabu, Mthunzi ukuthi bangamukele ukuthi nami ngiveze okubekwe uThixo kimi wow my life will never be the same again and ngihambe kahle ngidedela abanye ukuthi bayoveza okusezinhlizweni zabo ngigcine ngengoma ethi. Hlabelela meaning" Worship" pls ngicela sihlabelele sisebenzele izulu. , from now on sengi fulltime kuSphumelele i'm available for any event lapho ngidingeka khona and Joyous will always be my family but im nolonger a JC member thank you so much for unconditional love , Love Sphumelele (Ngibusisiwe ngingena ngibusisiwe ngiphuma okuhle noMusa kuyangilande) to those who always pray for me pls continue pray for me to those who didnt understand me trust me even me personal I dont understand me but God is using me in his own way for his Kingdom and to those who have problems dont for get problems are meant to make you see how strong you are but you can not see that during your trial so. Let us worship God in Truth and in Spirit and surely Goodness and Mercy shall follow us in Jesus Name Love you all!
    Like · Comment · 
Sphumelele alijiunga kwenye kundi la Joyous pamoja na waimbaji wengine wawili Charisma Hakenum pamoja na Kgotso Makgalema (ambao walishatoka Joyous) wakitokea kwenye shindano maarufu la "I want to Sing Gospel" la nchini humo likiwa chini ya Lindelani Mkhize mmoja wa viongozi wa Joyous ambapo Sphumelele alishika nafasi ya tano, lakini kutokana na kitu cha tofauti alichokuwa nacho katika uimbaji alipewa nafasi katika Joyous ambako alianza kuvunja ngome za shetani kuanzia DVD ya 13 ya Joyous aliyoimba wimbo Maye na Iququlwe. Hivi sasa mwimbaji huyo atakuwa akifanya kazi zake za uimbaji kama mwanamuziki wa kujitegemea

Soma habari zilizopita za mwimbaji huyu kwa kubonyeza Hapa

Tazama kazi ya kwanza ya Sphumelele akiwa na Joyous 

Joyous 16


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.