SOMO: AGANO LA DAMU (sehemu ya mwisho)

Toleo lililopita (bofya hapa kusoma) tulichambua vipengele muhimu vya; i) Kumsikiliza Yesu Kristo peke yake; ii) Kazi ya Roho Mtakatifu ni ambayo ni kuwasilisha kwetu anayosikia kutoa kwa Yesu Kristo. Leo naona tifikie hitimisho la mada hii kwa kupitia kwa ufupi tofauti zilizomo kati ya Agano la Kale na Agano Jipya, na jinsi itupasavyo kujenga fundisho la imani kwa kuzingatia mwongozo uliomo katika Agano jipya la damu ya Yesu:

Askofu Sylvester Gamanywa

Muhtasari wa tofauti kati ya
Agano la Kale na Agani Jipya

Mpendwa msomaji, wakati tunapohitimisha mada hii ya Agano la damu, sina budi nikupitishe kwanza kwa jumla kuhusu tofauti za maagano mawili yaliyomo katika Biblia. Kisha nitakuonesha tofauti zilizomo kwa kuzingatia vipengele maalumi li upate kujua ni kwanini inatupasa kujena fundisho la imani kwenye maandiko ya Agano Jipya badala ya Agano la Kale.

Kimsingi, Japokuwa Maandiko katika Biblia ni ya kitabu kilichounganisha ujumbe wa vitabu vyote, lakini iko tofauti kati ya maandiko kati ya Agano la Kale na yale ya Agano Jipya. Agano la Kale limeweka misingi inayoonekana kuwa kweli za Agano Jipya zinathibitishwa. Aidha Agano la Kale limesheheni nabii ambazo zimetimia katika Agano Jipya

Agano la Kale linaonyesha visa na historia za watu mbali mbali, wakati Agano Jipya linamlenga Mtu mmoja ambaye ni Yesu Kristo. Agano la Kale linadhihirisha ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi (sehemu ndogo ya neema); wakati Agano Jipya linadhihirsha neema ya Mungu kwa wenyedhambi (na kwa sehemu ghadhabu ya Mungu)

Agano la Kale linatabiri ujio wa Masihi (Isa.53), na Agano Jipya linamtambulisha Masihi mwenyewe (Yh.4:25-26) Agano la Kale limeandika Sheria ya torati, na Agano Jipya linaonesha jinsi Yesu kama Masihi alivyotimiliza sheria ya torati (Matt.5:17; Ebr.10:9)

Agano la Kale linajihusisha zaidi na taifa teule la Wayahudi; wakati Agano Jipya linajihusisha zaidi na Kanisa la Kristo (Mat.16:18)

Baraka za kimwili zimeanishwa katika Agano la Kale (Kumb.29:9), wakati Baraka zote za rohoni zimetolewa katika Agano Jipya (Efe.1:3)

Kwa kuwa ufunuo wa Mungu katika Maandiko ni endelevu, Agano Jpya linaweka mkazo kwenye kanuni ambazo zilikwisha kutambulishwa katika Agano la Kale. Mathalan, waraka kwa Waebrania unatafsiri jinsi Yesu alivyo Kuhani Mkuu wa kweli, na jinsi ambavyo anachukua nafasi ya dhabibu zote zilizotangulia kufanywa katika Agano la Kale kama kivuli

Mwana-kondoo wa Pasaka katika Agano la Kale (Ezr.6:20) anafanyika Mwanakondoo wa Mungu katika Agano Jipya (Yh.1:29). Agano la Kale linatoa sheria. Agano Jipya linaweka bayana kile ambacho sheria zilimaanisha zikionesha hitaji la wokovu na sio kwamba sheria ndio msingi wa wokovu (Rum.3:19)

Agano la Kale linaonesha jinsi paradise ilivyopotea kwa sababu ya Adamu; wakati Agano jipya linaonesha jinsi paradisho ilivyoreshwa kupitia Adamu wa pili, yaani Kristo. Agano la Kale linatangaza jinsi binandamu alivyotengwa mbali na Mungu kwa sababu ya dhambi (Mwanzo 3), na Agano Jipya linatangaza binadamu alivyorejeshwa kwa Mungu kupitia Kristo (Warumi3-6)


Vipengele vitano vya tofauti za
Agano la Kale na Agani Jipya

1.         Tofauti za kihistoria.

Vitabu vya Agano la Kale viliandikwa tangu enzi za Musa mpaka mwaka 400 K.K Hii ni sawa na miaka ipatayo elfu moja kuanzia wakati wa uumbaji wa ulimmwengu mpaka Wayahudi kurejea Yerusalemu chini ya Ezra na Nehemia. Maandiko ya Agano Jipya yaliandikwa kati ya miaka 50 B.K na 150 B.K

2.         Tofuati za kimwelekeo.

Agano la Kale limenaidka nguvu na matendo ya Mungu vikiashiria ujio wa Masihi. Agano Jipya linamfunua Yesu kama Masihi, likisimulia maisha yake na mafundisho yake kama msingi wa Kanisa na uenezaji wa Injli.

3.         Tofuati za kinabii

Sehemu kubwa ya nabii za Agano la Kale zililenga mambo yajayo na hazikuwahi kutumia baada ya mchakato wa maandiko ya Agano la Kale kukamilika. Agano Jipya linadhihirsha utimilifu wa nabii za Agano la Kale, zikiwemo zaidi ya nabii 300 katika maisha ya Yesu Kristo

4.         Tofuati za matendo ya ibada

Sehemu kubwa ya Agano la Kale inalenga ibada za hemani na hekaluni kama sehemu kuu ya mahali pa kuabudia. Humo ndimo yameanishwa mambo yote kuhusu dhabihu, sikukuu za kiibada na yote yenye kuhusiana na hayo. Katika Agano Jipya, Yesu alijitambulisha kuwa ndiye mlengwa wa ibada, akijitaja kuwa yeye ndiye njia, na kweli na uzima, na kwamba hakuna awezaye kuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwake (Yh.14:6)

5.         Tofauti za kiagano

Agano la Kale limejengwa kwenye torati ya Musa. Agano Jipya limeanza na “Agano Jipya” ambalo Yesu alikuja kuitimiza torati. Wayahudi na mataifa hawahitajiki tena kufuata torati ili kuhesabiwa haki; bali Yesu alitoa msamaha na uzima wa milele kwa wote wanaomwamini.

Na kwa mantiki hii, fundisho la imani kwa waamini linatakiwa kujengwa kwenye msingi wa maandiko ya Agano Jipya, na maandiko ya Agano la Kale yanabaki kama historia ya mambo yaliyotimizwa kwenye agano jipya.

MWISHO

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.