SOMO: CHOMBO CHA HESHIMA - PROFESSA V.N SIBIYA UFUFUO NA UZIMA

Mchungaji Dkt Josephat Gwajima na Professa Sibiya 


SOMO: CHOMBO CHA HESHIMA
Prof V.N Sibiya
Utabiri juu ya Ufufuo na Uzima


Imeandikwa; lakini jeshi lililotoka kaskazini nitaliondolea mbali nanyi, nami nitalifukuza mpaka nchi ya ukame na ukiwa; sehemu yake iliyo mbele itaingia katika bahari ya mashariki, na sehemu yake iliyo nyuma itaingia katika bahari ya magharibi; na uvundo wake utapanda juu, na harufu yake mbaya itapanda juu, kwa sababu ametenda mambo makubwa. (YOE. 2:20 SUV)

Mungu anasema kuwa hizi ndizo yakati ambazo adui atakimbizwa mbali na maisha yetu. Mungu amewapa nguvu watu wa Ufufuo na Uzima juu ya nguvu zote za giza. Huu ndio utabiri wa kinabii ambao Mungu ameuweka ndani ya moyo wangu juu ya Ufufuo na Uzima na nataka ujiandae kwaajili ya mambo makubwa yajayo.

Mstali wa 23 inasema : Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie BWANA, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi mvua ya masika, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, kama kwanza. (YOE. 2:23 SUV)

Sayuni maana yake ni mlima ambao Mungu anapatikana, ni mlima wa ishara na maajabu yanaonekana , ni kile ambacho hakiwezi kuigwa na watu wengine, inukeni sasa kwa utukufu wa Bwana kwa wakati wa uamsho wa mwisho kwasababu Bwana amejiinua kwa Neno lake kutoka kwa mtumishi wake aliyemsimamisha. Kila mtu ajiandae kwakutumiwa na Bwana kwasababu kila aliyetayari kutumiwa na Bwana ni chombo cha heshima.

Nimefanikiwa kusikia shuhuda mbali mbali za watu waliofufuka ufufuo na uzima na wengine hawakufufuliwa na mchungaji GWAJIMA bali watenda kazi wengine; hapa lipo jambo la kujifunza.
Huduma huanzia kwa mtu mmoja aliyemtegemea Mungu anayechukua maarifa kutoka kwa Mungu na kuyameza ndani yake na kuwapa watu wake, na wale wanaohamishiwa ule upako wa Mungu wanakuwa na uwezo aw kusambaza kutoka mtu mmoja hadi mwingine mpaka dunia yote.

Hivyo basi kile kitu ambacho Mungu amekiweka kwa Askofu Dr Josephat Gwajima inabidi kitoke ndani yake kiende kwa watu wengine, na wao wakipeleke duniani kote, hii ndio sababu watu wanaotakiwa wahahame kutoka Kuwa waongeza idadi kanisani kwenda kwenye washirika, na kutoka kuwa washirika Kuwa watenda kazi

Hatuhitaji watu ambao mbeba maono anaposema twende wanaanza kuongea mambo mengi na kuweka midahalo, tunatakiwa tuwe na watu ambao wanaushuhuda wa kufufua wafu na kuonyesha mfano jinsi walivyoomba mpaka wakafufua kwasababu mchungaji ndiye aliyewachoma sindano ya maarifa kuomba kwa jinsi hiyo na ndiyo jinsi ule moto uliokuwa ndani ya mchungaji kiongozi ulitembea kwa mtu huyu na Yule na Yule hadi ukamfikia aliyekuwa amekufa na kumfufua kutoka kwa wafu.

“Katika jina la Yesu mauti ya Biashara, ndoa, kazi, elimu na mauti yoyeto ile ninaikamata kwa jina la Yesu ninaingoa ninaamuru uzima wa Ufufuo na Uzima usambae kwenda kwenye kila nyumba.”

Hii ndio sababu huwa nawashangaa watu wengi ambao wanawanukuu wahubiri wa kwenye television na kuwadharau wahubiri na watumishi wakubwa wa Mungu walionao kila siku.

Ili ufanikiwe unatakiwa kutenda vile ambavyo unaona baba yako anatenda, unaona Kama baba yako anavyoomba na ile Roho inayotenda kazi ndani ya baba yako inahamia kwako na unaona matokeo yale yale.

Mstari wa 24 imeandikwa : Na sakafu za kupepetea zitajaa ngano, na mashinikizo yatafurika kwa divai na mafuta. (YOE. 2:24 SUV)

Ngano ni ishara ya kupewa mpaka ukatosheka, ni ishara ya kuridhika na kutosheka ulivyo navyo, ni ishara hakuna aibu tena, hakuna maumivu tena huta dharaulika tena, Mungu amlichagua kanisa hili kua ishara ya kuheshimika, wale ambao wamekata tamaa na magonjwa, na mashetani, na laana za familia watakapojifanya kuwa rafiki wa kanisa hili la ufufuo na Uzima na Baraka zake watachukua pia, na sio Tanzania peke bali Bara lote la Afrika na sio Afrika pekee ni Ulimwenguni kote.

Na Mungu ameniambia nikuambie leo nami nitakurudishia miaka yako uliyoipoteza.

Imeandikwa : Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. (YN. 10:10 SUV)

Kabla shetani hajakuua lazima akuibie kitu kwanza ndipo akuue “anaiba ndoa alafu anakuua, anaiba ujasiri halafu anakuuwa” . Unapokua unamshughurikia shetani ni vizuri kufuatisha huu utaratibu anaotumia kuharibu.

Nakuacha na ujumbe huu Leo ; chombo cha heshima mbele za Bwana.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.