SOMO: IJUE BIBLIA YAKO - MTUMISHI MADUMLABwana Yesu asifiwe sana…


Nataka nikujuze kidogo siku ya leo.
Siku ya leo nimeamua kukuandikia kuhusu kitabu cha ajabu ulimwenguni. Kitabu hicho ni biblia,biblia ni kitabu cha ajabu kwa sababu neno la Mungu huifadhiwa humo. Duniani vipo vitabu vingi chungumzima,lakini vyote huja na kupita mara,lakini biblia haipiti kamwe maana neno la Mungu ladumu milele.

Tunasoma;
“ Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele. ” Isaya 40:8

Hapa tunaambiwa,
Vitu tuvionavyo vinaharibika,vitu vyote chini ya jua huja na kuondoka,bali neno la Mungu litasimama milele.
Neno “ milele ” ni muda usiokuwa na kikomo. Hivyo neno la Mungu litasimama katika muda usio na kikomo.

Imeandikwa pia;
“ Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. ” Mathayo 24:35


Neno biblia limetokana na neno la kiyunani “ biblion” lenye maana ya makusanyo ya vitabu vya neno la Mungu yaliyovuviwa kwa pumzi ya Mungu aliye hai,ni maneno ya Mungu yenye uhai,yenye kufundisha,kuelimisha na kuadabisha sawa sawa na neno tulisomalo katika Timotheo;

“ Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ” 2 Timotheo 3:16

Haleluya…

 Biblia ina vitabu 66,
Agano la kale lina vitabu 39 na,
Agano jipya lina vitabu 27.


 Agano la kale lenye vitabu 39.
~Vitabu hivi 39 vimegawanywa katika makundi manne kama ifuatavyo;


(i) kundi la vitabu vya Pentateuko,(vitabu vya sheria,torati)
~ Kundi hili la vitabu vya torati huanzia kitabu cha MWANZO mpaka kitabu cha KUMBUKUMBU LA TORATI. Sheria zote zilizoandikwa katika vitabu hivi ni sheria zilizokuwa ziki zikiwataka watu wazishike.Hata hivyo watu wa agano la kale walishindwa kuzishika sheria hizo,na Yesu akaleta agano jipya Yeremia 31:31-32


(ii) Kundi la vitabu vya historia.
~ Kuanzia kitabu cha Yoshua mpaka Esta.(iii)Kundi la vitabu vya hekima na vitabu vya mashairi.
~ Kuanzia Ayubu mpaka wimbo ulio bora.(iv)Kundi la vitabu vya manabii wa dogo,na manabii wakubwa.
~ Kuanzia Isaya mpaka Malaki.Agano la kale lenye vitabu 27.

~ Agano jipya nalo limegawanywa katika makundi manne kama ifuatavyo;
(i)Vitabu vya injili.
(ii) Matendo ya mitume
(iii)Nyaraka za Paulo.
(iv)Ufunuo.

Nyaraka za mtume Paulo ziliandikwa kama mnamo mwaka 48. BK.
Ufunuo ndicho kitabu cha mwisho cha agano jipya,mnamo mwaka wa 100 BK kiliandikwa.


Mpangilio huu haukulenga muda wa kitabu kilipoandikwa na Roho wa Bwana. Maana kama mpangilio huu ulilenga muda basi ni dhahili kabisa kitabu cha Ayubu kingekuwa katika mtililiko wa juu,yaani kingepangwa juu ya vitabu vingine au kingepangwa baada ya vitabu vya torati kwa sababu kitabu cha Ayubu kimeandikwa zamani kuliko vitabu vyote.


Katika biblia ya Kiyahudi,vitabu vyake ni hivi hivi,lakini mpangilio wake hutofautiana kidogo maana wao wamevigawa vitabu hivi katika makundi matatu tu;
~ Sheria (torati)
~ Manabii
~ Maandishi.

Haleluya…


Lugha zilizotumiwa katika biblia.


~ Biblia katika agano la kale limeandikwa sehemu kubwa katika lugha ya Kiebrania,ingawa yapo mafungu ya maneno yaliyoandikwa katika lugha ya Kiaramu.
Mfano katika vitabu vifuatavyo
Ezra,
Yeremia na,
Danieli
Vimekutwa na mafungu ya lugha ya kiaramu. Hii ni kwa sababu kiaramu ilikuwa ni lugha iliyotawala katika uhamisho wa Baleli.

~Lugha iliyotumika katika agano jipya ni lugha ya Kiyunani ambayo ilikuwa ni lugha ya ulimwengu wote wa dola ya Kirumi.


Hata hivyo biblia ilikuja kutafsiriwa kwa mara ya kwanza ili kuwezesha uelewa kwa watu wengi wa kila taifa. Tafsiri ya kwanza inayojulikana ni Septuaginta. Hii ilikuwa ni tafsiri ya kutohoa maneno kutoka katika lugha ya Kiebrania kwenda katika lugha ya Kiyunani kama jinsi vile agano la kale lilivyoandikwa katika lugha ya Kiebrania.
(Tafsiri hii ilifanyika mnamo kama katika mwaka 280 KK,huko Iskanderia nchini Misri)


Ubora wa neno la Mungu katika biblia umedhibitiswa na Mungu mwenyewe. Roho mtakatifu hufanya kazi katika neno lake. Hivyo neno la Bwana limevuviwa na Roho mtakatifu,li hai jana,leo hata milele.


Kwa mawasiliano yangu;
Mtumishi Gasper Madumla
0655-11 11 49.
Mch. Gasper Madumla,
Beroya Bible fellowship church.

UBARIKIWE.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.