SOMO: KURUDUSHA WALIO IBIWA - MCHUNGAJI GWAJIMA

Mchungaji Josephat Gwajima
SOMO: KURUDUSHA WALIO IBIWA

Ezekiel 13:18 “Useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe? Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo. Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege. Na leso zenu nazo nitazirarua, na kuwaokoa watu wangu katika mikono yenu, wala hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Kwa kuwa ninyi mmemhuzunisha moyo mwenye haki kwa uongo, ambaye mimi sikumhuzunisha; na kuitia nguvu mikono ya mtu mbaya, hata asigeuke, na kuiacha njia yake mbaya, na kuhifadhika; basi, kwa sababu hiyo ninyi hamtaona tena ubatili, wala kutabiri mambo; nami nitawaokoa watu wangu katika mikono yenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.”

Tunaona kuna watu wanaoshona hirizi na kuziwinda roho za watu. Imeandikwa nitakulinda na mtego wa mwindaji. Kuna roho za watu ambao walikufa lakini haikuwapasa kufa na kuna watu ambao walitakiwa kufa lakini hawajafa. Mungu anasema kuna watu ambao hawakupaswa kufa lakini wamekufa na watu wamesema uongo kwamba ‘ni kazi ya mwenyezi Mungu haina makosa mwacheni alale kwa amani’ lakini sisi tunasema hapana kwasababu Mungu ametubariki sana kwa miaka sabini akituzidishia sana miaka themanini ya kushi. Lazima walioibiwa warudi kwa jina la Yesu.

KUNA MISIBA MITATU AMBAYO YESU ALIHUDHURIA

1. “Msiba wa waliokuwa wamebeba geneza wanakwenda malaloni” alipokutana nao akawaonyesha tofauti kati ya ku. Yesu akamwambia Yule kijana “toka ndani ya geneza” na Yule kijana akatoka.
2. “Kwa binti Yairo” alipofika pale akawaambia anapoingia kule ndani wengine wabaki nje na akamchukua Petro ambaye ni “mwalimu wa matumaini” Yakobo ambaye ni “mwalimu wa imani” na Yohana ambaye ni “mwalimu wa upendo” na kina Tomaso wakabaki nje. Hii inamaanisha kuna wanafunzi wa Yesu ambao mambo ya kufufua hayawahusu. Alipoingia ndani akawaambia huyu mtu hajafa bali amelala, akamwabia Yule binti simama na Yule binti akasimama katikati ya vile vicheko vya wale watu.

3. Yesu aliwaambia kwamba amelala na kawa na manno kwamba hakuwa amekufa bali amelala na Yesu akaamua kuwangojea wakati wanakwenda kumzika mtu mwingine na akamfufua na hawakumwamini tena akasema kwavile alivyomfufua Yule aliyekuwa amekufa alisema amelala na huyu naye alikuwa amelala na Yesu akawangojea kwa mtu mwingine ambaye ni Lazaro aliyeuugua lakini Yesu hakwenda umponya, Lazaro akafa siku tatu na akaanza kuoza ndipo Yesu akaenda na alipofika pale akamfufua Lazaro, akasema “Lazaro njooo huku nje” inamana Lazaro alikuwa ndani ya shimo amefichwa amefungwa, na Lazaro akasimama na funza waliokuwa wameanza kumtoka na harufu iliyokuwa inamtoka vote vikapotea Yesu akasema mfungueni mwache aende zake. Hii inamaanisha kwamba Kazi ya kufungua watu ni Yetu.

4. Mitume na manabii walfufua wafu.
Eia alimfufua mtu 1Wafalme17:18,
Elisha alimfufua mtu 2Wafalme4:10-31
Paulo alimfufua tu aliyeanguka toka ghorofa ya tatu
Petro alimfufua dorkasi.

1 Wakorintho15: 14 “Tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure. Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi. Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka. Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu. Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.”
Mathayo10: 8 “Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.”
Yohana11: 23 “Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?”

YESU ALIFUFUA KWA AINA TATU.
1. Waliokufa siku hiyohiyo.
2. Wanaokwenda malaloni
3. Waliokufa na kuzikwa.

AINA ZA MISUKULE

1. Mtu anajisikia kuumwa na kumbe wachawi wamefanya bihashara za kuuza miili ya watu na roho za watu na wamekuwepo muda mrefu, mtu huyo anaumwa mpaka anafariki na wachawi wanaweka gogo lililonuiziwa livae sura ya aliyefariki “malaika wachafu wa giza wanawezakujigeuza kuwa kitu chochote” na wanamweka ndani ya geneza watu wanaopita wanaona kuwa ni kitu cha kawaida hawaoni kumbe wanakenda kuzika gogo au kitu chochote. Kuna matajiri unaowaona leo ndio wanaowachukua watu hawa kwenye shughuli zao mfano kutengeneza lambalamba.

2. Watu waliolala na kuitwa usiku kwa sauti na wanapoitikia wanakuwa wamechukuliwa na wanapochukuliwa wanaharibiwa akili zao na kwenda kutumikishwa kwa kazi gumu na nyumbani kwao wanajua amekufa kumbe yupo mjini au mahali amafanya kazi nzito na ngumu.

3. Mashetani yanaweza kujigza na kuvaa umbo lolote na hao wanakopi sura na kuwa kama binadamu na mtu mwenyewe anachukuliwa na kubakia jini ambalo linaonekana halijui kitu na kama ni mtoto anakuwa hajui kitu chochote anachofundishwa kumbe ni jini lililovaa mwili.

Unamkuta mtu amedondoka chini na akija kuamka anakuwa ni mwingine, unakuta mtu anaugua na akija kuamka ni mwingine.

Lazima watu wote walioibiwa, bihashara zilizoibiwa, nyota zilizoibiwa, kazi zilizoibiwa zirudi kwa jina la Yesu.

4. Mtu ni roho yenye nafsi inayokaa ndani ya nyumba na nyumba inaitwa mwili. Ndio maana roho ya mtu inapotoka ndani ya mtu, mtu huyu anaitwa amekufa na roho ya mtu inapokuwa imerudi ndani ya mwili wa mtu mtu huyo anaitwa amefufuka. Wachawi wanachukua roho yake wanaondoka nayo na kwa kawada roho ya mtu ikitoka mwili unakuwa haufanyi kazi sasa wanapokuja kuchukua roho ya mtu wanakuja na roho ya Shetani “pepo” na mtu mwnyewe anachukuliwa kwenda kufanya kazi za kusababisha ajali na majanga mengine na kutumikishwa wanakuwa kama mapepo.

Ufunuo18: 9 “Na hao wafalme wa nchi, waliozini naye na kufanya anasa pamoja naye, watalia na kumwombolezea; wauonapo moshi wa kuungua kwake; wakisimama mbali kwa hofu ya maumivu yake, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu, Babeli, mji ule ulio na nguvu! Kwa kuwa katika saa moja hukumu yako imekuja. Nao wafanya biashara wa nchi walia na kumwombolezea, kwa sababu hapana mtu anunuaye bidhaa yao tena; bidhaa ya dhahabu, na fedha, na kito chenye thamani, na lulu, na kitani nzuri, na nguo ya rangi ya zambarau, na hariri, na nguo nyekundu; na kila mti wa uudi, na kila chombo cha pembe, na kila chombo cha mti wa thamani nyingi, na cha shaba, na cha chuma, na cha marimari; na mdalasini, na iliki, na uvumba, na marhamu, na ubani, na mvinyo, na mafuta ya mzeituni, na unga mzuri, na ngano, na ng'ombe, na kondoo, na farasi, na magari, na miili na roho za wanadamu.”

Unaona mfanya bihashara anastawi lakini wewe unasinyaa kumbe unafishwa bihashara mahali. unamwona mtu yupo nyumbani kumbe ni mwili wake tu lakini roho yake inafanya kazi mahali. Mungu alipomuumba mtu alimbariki ama mikono, ama uso, ama akili na wachawi hawa wanaamua kumchukua na nyota yakewanaifanyia bihashara.

Utamkuta mtu ambaye amechukuliwa roho yake msukule unagundua mtu huyo hayupo na ukimwombea utaona anarudi na anapona kabisa.
Isaya42:22
Kumbukumbu l a torati 18 “ Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako. Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako.”

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.