SOMO: MAUTI IMEMEZWA - MCHUNGAJI KILIMA UFUFUO NA UZIMA TANGA

Mchungaji John Kilima

SOMO: MAUTI IMEMEZWA
Mauti ni roho, mauti yaweza kumezwa na roho inaweza ikamezwa na isionekane kabisa. Roho yaweza kugeuka na kuwa hata chakula ukala na kupita matatizo.
Ufunuo 6:7
Na alipofungua muhuri ya nne nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wanne akisema, njoo nikaona na tazama, farasi wa rangi ya kijivu jivu nay eye aliyempanda jina lake ni mauti, na kuzimu akafuatana naye, kuzimu yaweza ikamezwa.
1Wakorintho 15; 33-

Msidannganyike, mazungumzo mabaya huharibu tabia njema, tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu.
kama umeokoka ni lazima ulisome neno la Mungu kwa maana pasipo kutenda hivyo kwa mtu uliyeokoka utakuwa hatarini kuliko mpagani.
Shetani hafanyi kazi hadi apewe nafasi efeso 4:27 wala usimpe ibilisi nafasi,
Dhambi, nguo za uchafu humpa shetani nafasi, shetani hutenda kazi akiwa amepewa nafasi, hata kwa Ayubu, shetani alipewa nafasi ndio maana akamjaribu. Hatima ya mtu huanzia tumboni mwa mama yake, hata jina humsababishia mtu matatizo, pia nguo ulioyo achiwa huweza kuwa ni sababu ya matatizo yako, dhambi humsababishia mtu matatizo katika maisha yake, acha dhambi, acha mila ya kufagilia makaburi,

Mauti ya maisha yako, mauti ya ndoa, biashara lazima itaamezwa leo Kwa jina la Yesu,
Wanafufuliwaje wafu? nao huja kwa mwili gani?
1wakorintho 36
Ewe mpumbavu! Uipandayo haihuki, isipokufa nayo uipendayo, huupandi mwili ule utakaokuwa,ila chembe tupu ikiwa ni ngano au nyingineyo;lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake, nyama yote si nyama moja; ila nyingine ni ya wanadamu nyingine ni ya ndege, nyingine ya samaki. 

Fahali ya kitu cha kwanza ni tofauti na kile kitakacho ota.
Mwanadamu ni Roho nayo iko ndani ya nyumba na nyumba hiyo huitwa mwili roho ikitoka ndani ya mwili huwa kitu kingine, na fahari ya mwili wa duniani ni tofauti na mwili wa mbinguni
1wakorintho 15:40

Tena kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani, lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali. Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi na nyingine ya nyota maana kuna tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika, hupandwa katika udhaifu, hufufuliwa katika nguvu, hupandwa mwili wa asili, hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili na wa roho pia uko.
Nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu, wala uharibifu kurithi kutokuharibika, nawaambieni siri , hatutalala sote lakini sote tutabadilika..
Mavazi pia humsababishia mtu kuwa katika magereza ya dhambi na kuwa kifungoni
Tunabadilishwaje?

Kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika, sharti mwili huu uharibikao uvae kuto haribika
Mauti inakufatilia kwa sababu hujui inakuwaje

Mauti imemezwa
Mtu anapotea
Mtu anapotea ghafla maana yake mtu huyu mauti imemmeza, maana hata ukifukua makaburini hukuti chochote,
Yesu akawa wa kwanza kuimeza mauti
Mathayo 28:1-15
Uchungu wa mauti ni dhambi, kama mtu ukiwa katika sheria ya tolati na wale waliomwamini Yesu mauti yao huwa ni tofauti.walinzi pia huwekwa ili wakulinde usiweze kutoka katika kifungo ulichonacho..
Marko 16
Kuhusu ufufuo, mabari za Bwana Yesu wakati anafufuka.
Bwana Yesu yupo leo anaenda kuvingirisha jiwe lile lililo katika maisha yako, Yesu mwenyewe atashughulika, anza leo kupita katika mto Yordani na matatizo yote yatapita, mtu aliyefanikiwa aliamua kupita kwenye jangwa na kwa Yesu kuna milima na mabonde na kila palipo palizwa patasawazishwa kwa jina la Yesu

Jinsi mauti ilivyomezwa
Yesu alikuwa wa kwanza kuimeza mauti kwa kufufuka kwake. Mwili aliovaa Yesu baada ya kufufuka ni mwili uliobadilishwa ndio mana uliweza kutokea kwa sura tofauti.
Luka 24:1-12
Hata siku ya kwanza ya juma ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari, wakilikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi, wakaingia wasiuone mwili wa Bwana Yesu, hao waliwaambia mitume habari ya mambo hayo. Maneno yao yakaonekana kuwa kama upuuzi kwao, wala hawakusadiki, lakini petro aliondoka akaenda mbio hata kaburiniakainama akachungulia ndani, akaviona vile vitambaa vya sanda tu: akaenda zake akiyastaajabia yaliyotukia.
Roho ina tabia ya kuufunika mwili ili ili usionekane, mwili waweza kufunikwa na mauti.
Lazima utoke katika gereza lolote ambalo linakushikilia kwa jina la Yesu, gereza la mauti ya aina yoyoyte , ya kazi, ya ndoa, ya biashara, ya afya, laana na kila aina la gereza ambalo linakushikilia lazima utoke.
Yesu amerudi ili akuokoe, liko tumaini, mauti imemezwa, mauti inaweza ikatengenezwa na ikawekwa kaburini.
2Wakorintho 12; 2
Namjua mtu mmoja katika kristo, yapata sasa miaka kumi na minne,(kwamba alikuwa katika mwili sijui, kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua)
Ukishinda rohoni ni lazima ushinde na mwilini, ushindi huanzia rohoni.

AMEEN
UFUFUO NA UZIMA
DUGA MWEMBENI -TANGA
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.