SOMO: UHUSIANO WA VITI VYA ENZI NA MAFANIKIO YAKO (3) - MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE

Mwalimu Christopher MwakasegeUHUSIANO WA VITI VYA ENZI NA MAFANIKIO YAKO

Mahali: Viwanja vya Jangwani

Mnenaji; Mwalimu  C.Mwakasege

Kusoma sehemu ya 1 na 2 Bonyeza Hapa
Endelea na somo kama lilivyofundishwa siku ya 3 ya semina hiyo.


Matendo 12:1 -4 - 1 Panapo majira yale yale Herode mfalme akanyosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa.

2 Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohana, kwa upanga.

3 Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro. Siku hizo zilikuwa siku za mikate isiyochachwa.

4 Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu.


* Habari hii ya watumishi wa Mungu, Yakobo na Petro, Yakobo aliuwawa kwa upanaga, Herode alipoona watu wamefurahi akamkamata na Petro

* Baadhi ya maswali ambayo hawa watumishi wangekuwa na nafasi ya kumuuliza yesu wange uliza, ni kama yafuatayo

* Yakobo baada ya kuuwawa na kufika mbingunu akikutana naYesu, angeweza kuuliza "kitu gani kimetokea nimeuwawa wakati nakutumikia? malaika wako walinzi walikuwa wapi? , Ule upako ulioweka nandi mwangu umeenda wapi usinisaidie?.

* Yakobo pia angeuliza kwanini mimi, wakati ulipoondoka Yuda ndiye aliyepotoka tukamchagua mathia, wakati tunaanza tu huduma ktk wanafunzi kumi na mbili kwa nini mimi?

* Unadhani Yesu atamjibu vipi?. Si jui kwa upande wako?

* Jambo la Petro kufungwa lilikuwa limemuuzmiza sana, Petro alikuwa amelala wakati Paulo na sila walikuwa wakiomba gerezani katika shida kama ya Petro. Inawezekana Petro alikuwa akiwaza kwa maswali akiwa jela, kosa langu ni nini?

* Petro angeweza kuuliza kama yakobo ule upako ambao hata kivuli changu kilikuwa kinaponya kwa nini haukunisaidia hata kutiwa gerezani?., Angweweza kuuliza pia kwa nini mimi, Swali lingine Herode amepata wapi ujasiri wa kuharibu kazi hii ya Mungu?.

* Swali la Kumuuliza Yesu, herode ni nani hata akazuia kazi ya Mungu "Panapo majira yale yale" inamaanisha kuna jambo lilitokea kabla, unganisha na "siku hizo nabii agabo..." unganisha na Mdo 12:25....Inamaanisha na huduma ya kusaidia jamii kipindi cha njaa ilikoma wakati Yakobo anauwawa "majira yale yale".

* Hudumu ya Barnaba na Sauli nayo ilikoma mpaka herode alipouwawa

* Swali kuna shida ganai hata herode akataze huduma hii ya chakula kwa watu isifanywe .,Je kama wangefanya wengine angeizuia?

* Twende Mdo 6: kwa habari ya Stephano...sasa nenda na stephano mbinguni akipokewa na yesu na kuwa na maswali.

* watu huwa wanaondoka na maswali, maana kwa habari ya tajiri na laziro, tajiri alipata nafasi ya kuuliza maswali kule

* Swali ambalo stephano angeuliza, kwa nini mimi nipigwe mawe wa kwanza kati ya situ tuliochaguliwa na kuwekewa mikono (watu 7). Kwa nini mimi stephano?

* Unapokwenda kwenye mazishi, kuna baadhi ya wachungaji huwa wanaomba juu ya anayefuta baada ya aliye kufa, ni wangapi wanaweza sema wako tayari?

* Petro alimkemea Yesu lakini baadae aakamgeuka kwa ajili ya woga

* Kwa nini stephano alichaguliwa na kupigwa mawe, Mdo 6: 8...Stephano na upako...Atamuuliza Yesu inakuakuaje ule upako na neema niliyokuwa nayo havikunisaidia?

* Kuwa na upako haina maana kwamba utakulinda,


Angalia mdo 7: 54-55, "Basi waliposikia maneno haya, wakachomwa mioyo, wakamsagia meno.

55 Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu.

56 Akasema, Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu."


* Kwa nini anoe mbingu zimefunguka na asipate msaada?.

* Mbingu zimefunguka kwa ajili ya nini? , Stephano atauliza, Je kuna mahali nilipokukosea hata YESU usinisaidie wkati napigwa mawe?.

* Kumbuka Huduma ya stepano ili kuwa ndio kwanza inaanza, swali ambalo watumishi wengi huwa wanajiuliza ni hili "kwa nini huduma yangu inapochanua ndio inakumbana na vita kali?"....."

* Stephano alikuwa na maswali mengi, Biblia inasema mdo 6:8-13..na 7:1

*

Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu.

9 Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;

10 lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye.

11 Hata wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu.

12 Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza.

13 Wakasimamisha mashahidi wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati;

1 Kuhani Mkuu akasema, Je! Mambo hayo ndivyo yalivyo?


* Stephano alipoulizwa swali hilo akawachapa injili na mioyo ikachomwa, aliposema mbingu imefunguka wakamtoa nje na kumuua

* Swali, hivi YESU hizi sinagoni ni za kwako, na huku wananisimamishia mashahidi wa uongo?, kama sinagogi nila kwako wanapata wapi ujasiri wa kunipiga mawe?

* Kama Wewe ni Yesu ungejibu nini?

* Hebu tumuangalia Antip, Ufunuo 2: 12-13

*
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili.

13 Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.

* Achana na kiongozi anayeandika, twende kwa Antipa, kama angepata kuuliza maswali angeuliza ule upako, kwa nini haukunisaidia wakati wananiuwa kama shahidi?, lingine kwa nini niuwawe kanisani kama shahidi wako?. wale mashahidi wengine wakisikia nimekufa watapata wapi ujasirii wa kuendelea wakati nimeuwawa ndani ya kanisa?

* Unaniita mimi mwaminifu wako lakini wamenua, kumbuka barua iliandkwa baada ya antipa kufa/ ,Lazima angeuliza hawa ni wako kweli? . angeuliza pia kwa nin mimi?

* Na mimi (MWL) nilikuwa nanyongeza ya maswali mawili, 1. kwa nini kanisa lina mamlaka juu ya mapepo lakini inapokuja kwa wenye mamlaka wanashindwa?. mfano wakikutana na askofu mpinzani watu wanahama kanisa?

* Tulikuwa Tanga wakati ule habari za amboni ndio zimeanza, wengi wakasema mnaenda wakati ni mgumu(shamba lilikuwa gumu)?. Shamba likiwa gumu mwombe Bwana Yesu akubadilishie jembe.Pamoja na changamoto zile, tulifanya mkutano mkubwa sana Tanga ambao hatujawahi fanya tena Tanga

* Kwa nini kanisa liwe na mamlaka ya kukemea pepo, lakini wakikutana na upinzani wanaanza kukimbia?..hili swali nilimuuliza Bwana Yesu

* Kwa nini unaweza kemea mapepo mahali pengine mfano kanisani, lakini kwa kaka mkubwa au baba yako au kwenye ukoo wenu unakimbia?

* Nikauliza swali la pili "Kwa nini wakati wa mapambano nguvu zinapungua na watu wanakimbia".

* Swali lingine nililouliza "Luka 10:2 Akawaambia, Mavuno ni mengi, laki ni watenda kazini wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake" Bwana umeona watu wasio na mchungaji, ukatupa nafasi ya kuomba watenda kazi, Kwa nini kama watenda kazi ni wachache wewe unawaacha hawa wachache wauwawe?'

* Nilimuuliza haya maswali Bwana Yesu, Naye amekuwa kinijibu hatua kwa hatua na kunipa ufunuo juu ya Kiti na mambo mengine

* Ufunuo 13:2, 7 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.

Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.

8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.

9 Mtu akiwa na sikio na asikie.

10 Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.


* Haya maneno yanafana na Kanisa la Pergamo ufunuo 2:17

* Yeye aliye na sikio na asikie

* Kuna mafundsiho ambayo Mungu ameyaficha hadi kanisa litakapo kaa mkao wa kusikia....

* Shetani anatumia watu akifika mahali, akiwapata anawapa nguvu na kiti chake, Akishampata mtu anatumia vitu vyote vinne ili Kupiga vita watakatifu, kumiliki makundi kwa makundi na anawapa nguvu zake na mamlaka

* Kiti cha enzi kinampa aketiye mamlaka ya kieneo, Biblia inasema shetani kama simba aungurumae, Ukimwangalia simba akinguruma anaweza maanisha ananjaa akitafuta cha kumeza, Kama unaangaliaga zile documentary za wanyama, ukipata nafasi ya kumwangalia Simba

* Simba dume huwa anatabia ya kujitengea eneo atakalokuwa akiwinda (territory) (anajicholea mpaka), simba dume mwingine akiingia anapigwa.

* Jaribu kuwa na mimba ya maono ya Mungu halafu uzalie kwenye uwanja wa shetani, uone?. Ni kama Swala anapozaa huku simba Dume yuko pembeni!.

* Unapoanza kuwa tishio, shetani anatafuta kila kitu ili aweze kukumaliza, na mara nyingi atatumia kiti alichowapa wenye mamlaka.

* Wakristo wengi hawajui kuwa kuna mamlaka juu ya pepo na mamlaka juu ya eneo?.

* Wakati wa kipindi cha Petro walikuwa wanapambana na kiti cha Herode, Wakati wa herode the great (kipindi Yesu anazaliwa), harode alidanganya ili ajue habari za Yesu, na alipokosa habari aliwuwaa watoto wengi kwa kumwinda Yesu tu.

* Yohana mbatizaji alikuwa tishio kwa herode shetani akafuta mwanya akamwua> kwa nini? kwa sababu akisha uwa anawaitishia waliobaki hai

* Stephano alikaa juu ya kiti cha Musa, Kiti cha Musa kinasimamia sheria na Kiti cha Yesu kinasimamia neema, kibali...kiti ndicho kilicho muuwa stephano

* Shetani akishaingia kwenye eneo na mamlaka wakristo huwa wanaishiwa nguvu

* Wakati wa kipindi cha Antipa, kiti cha enzi kilisimama

* Wakati mwingine utasikia manano kama pale unapambana na ofisi na si mtu?.

* Stephano alikuwa anashindana na wakuu wa dini waliokuwa wamekaa juu yakiti cha musa

* Kiti cha neema ni tishio juu ya kiti cha Musa

* Cheki mamlaka iliyopo juu ya wakuu wa dini kanisani inakuwa kama kiti cha Musa cha sheria, kila kitu ni sheria na neno lao mara nyingi linakuwa ni fainal!.

* Wakati huduma yako inapoanza kuchanua unapoona upinzani jinsi unavyoinuka, maswali yanaibuka .

* Kwa nini mimi tu ndio napata shida Tu?. Si kila mtu atapata shida kama ya kwako isipokuwa ameshakuwa tishio kwa shetani

* Nilipata taarifa wakatifulani mtu akiniambaa amepata taarifa kwamba kuna mtu alisema siku nikipata nafasi nitamuua Mwakasege, wakamwuliza ni kwa nini yeye akasema sijui lakina na hasira nae", nikajichunguza nikagundua simjui na wala sijawahi kugombana nae...Wale walioniletea taarifa wakaomba baada ya muda tukasikia amekufa kifo kibaya

* Usije fikiria kila mtu anaysema amen anasapoti kazi ya Mungu, wengi wanahasira nawe

* Lile joka limeachilia kitu ndani...

* Inawezekana kunawatu wamesima na kutoa ushahidi wa uongo juu yako nawe umekata tamaa....Mfalme Agripa alisema sioni kosa la Paulo ila siwezi kumfungua

* Wakti unavita ofisini,ukishaona bosi kakuita pembeni na kukwambia sio mm ila ofisi, ujue ni kiti!.


* Shetani hapambani na wewe bali anapambana na kilichopo ndani yako, hana shida na Stephano bali anashida na Kiti.

Litaendelea Jumatano ijayo… kwa undani zaidi wasiliana na wahusika ili kujipatia CD
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.