SOMO: YESU NI MKATE WA UZIMA - KING SAMYESU NI MKATE WA UZIMA

BIBLIA INASEMA YESU SHETANI ALIKUJA KUMJARIBI NA JARIBU LA KWANZA LILIKUWA HIVI
Luka Luke 4:3
Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate
YESU ALIMWAMBIA SHETANI WEWE UTAISHI KWA MKATE, ILI LILIKUWA FUMBO KWA SHETANI HAKUJUWA,HATA KWA WATU BADO NI FUMBO LAKINI LEO NATAKA NI KUONYESHE ILI SHETANI HASIKUTESE TENA,
MATHAYO 6:11 YESU ALISEMA MSALIPO SEMENI UTUPE MKATE WETU WA KILA SIKU,JE NI KWELI ALIKUWA ANAMANISHA MKATE WA UNGA WA NGANO?WATU WENGI WAMEKUWA WAKIFIKIRI ALIKUWA ANAMANISHA HIVYO, LEO NA KUAMBIA HAPANA

NINI MKATE WAKO WA KILA SIKU NI NENO LA MUNGU YESU NDIYE MKATE ALISEMA HIVI
MATHAYO 26:26 Akatwaa MKATE akaubariki akawapa akasema kuleni huu ni mwili wangu,
JARIBU KUONA MUNGU ALICHOWAMBIA WANA WA ISRAEL KWAMBA PAMOJA NA KULA MANA HUTAISHI KWA HIYO MANA BALI KATIKA KILA NENO LITOKALO KATIKA KINYWA CHA MUNGU
Kumbukumbu la torati Deuteronomy 08:3
Akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha BWANA
ANGALIA YESU ANAJIFUNUA KUWA YEYE NDIYE CHAKULA YAANI NDIYE MKATE KWA HIYO YESU NDIYE MKATE WAKO WA KILA SIKU HUWEZI KUISHI PASIPO NENO LA MUNGU NDIYO MAANA WATU WENGI SANA WANAPOTOKA KWENDA KWENYE MISHIHULIKO YAO WANAPATWA NA MABAYA KWA SABABU HAWAJUI MKATE WAO WA SIKU HIYO NI NINI,MKATE WAKO WA KILA SIKU NI NENO LAKE
NDIYO MAANA ALIMWAMBIA YOSHUA NENO LA KITABU HIKI LISITOKE KINYWANI MWAKO ULITAFAKARI MCHANA NA USIKU
JOSHUA 1:8

JE WEWE UNAO HUO MKATE KILA SAA?LAZIMA UUJUWE MKATE WAKO WA KILA SIKU NINI
Yohane John 06:31
Baba zetu waliila mana jangwani kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili wale.
35 Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe
NDUGU YANGU YESU NDIYE MKATE WAKO WA KILA SIKU KWA HIYO KAMA SI MSOMAJI WA BIBLIA USITEGEME JARIBU LINAPOKUJA MBELE YAKO WAKATI WOWOTE UTAWEZA KUSHINDA YESU ALIJUWA YEYE ANAISHI KWA NINI NDIYO MAANA SHETANI HAKUPATA NAFASI KWAKE


Yohane John 06:50
Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni, kwamba mtu akile wala asife.
51 Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.
UKWELI HAKUNA MTU ALIYEKULA CHAKULA HIKI HAKAFA AU SHETANI AKAMSHINDA MAGONJWA YAKAWA SEHEMU YAKE HAKUNA,
TANGU NILIPOKULA MIAKA 20 ILIYOPITA NA NAZIDI KULA SIJAWAI KUUGUWA NA WALA SINA MATEGEMEO YAKUUMWA WALA KUFA
NDUNGU YANGU YESU NI MKATE ULIO HAI
Ezekieli 3:2
Basi nikafunua kinywa changu naye akanilisha lile gombo
NDUGU YANGU KATIKA KRISTO YESU YEYE AKUPE UWEZO WA KULA MWILI WAKE ILI USIFE KATIKA JINA LA YESU AMEN

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.