UJUMBE MAALUMU KWA WASIO OA AMA KUOLEWA KUTOKA KWA MCHUNGAJI

Ujumbe huu ni maalumu kwa wasio oa ama kuolewa kama ulivyotolewa na mwanzilishi pia mchungaji wa kanisa la NewSpring lililopo kwenye mji wa Anderson nchini Marekani, mchungaji Perry Noble, kama ilivyoandikwa kupitia kwenye mtandao wa Kikristo wa Christian Post

Kuna watu wengi wapweke siku hizi duniani, naelewa ugumu wa kuwa mpweke, sikufunga ndoa mpaka nilipokuwa na miaka 28. Natumaini leo kupitia maneno manne yafuatayo yatakutia moyo kama bado hujaoa au kuolewa.

#1 - Subira

Ukikimbilia kwenye ndoa, utajaribiwa kutaka kutoka kwenye ndoa wakati mkeo anaonekana kama ameacha kukupa kile ulichokuwa ukitarajia. Kuwa mpweke sio ugonjwa, ni kipindi ambacho Bwana atakufundisha mambo mengi kuhusu wewe na watu wengine kama tu utwakuwa na subira na kushiriki pamoja naye katika kipindi hicho.

#2 - Harakati
Uamuzi sahihi kwasasa kwa mtu ambaye hajaoa au kuolewa ni uamuzi wa kumfuata Yesu sikh zone za maisha yako. Imekuwa kawaida kwa watu wanaofanikiwa kuingia katika mahusiano kunasababisha wahusika kuacha kumtazama Yesu. Hata hivyo, kumbuka kama mtu atakutoa katika uhusiano wako na Yesu kuliko kukusogeza karibu naye, ni uhakika kwamba uhitaji kuwa na huyo mtu.

#3 - Shauku
Binafsi jiulize hili swali: Kama Mungu akikupatia mtu sasa hivi je utakuwa baraka kwake ama kwao au utakuwa laana?. Kuwa mkweli na nafsi yako kujibu hili swali. Kama unaona mwanya kwenye maisha yako unaosababisha kuwa laana usivunjike moyo, zaidi hivyo vitu viwe kama changamoto ya kumuuliza Yesu kubadili moyo wako na kuufanya uwe na hamu ya kumjua Kristo, ambaye ni pekee anayeweza kubadili laana kuwa baraka.


#4 - Mtazamo
Kumbuka hii Mungu ni mwema na hutaka mambo mazuri yatokee kwa watoto wake. Haijalishi mipango yako uliyopanga, Mungu anakuwazia mema. Mda wowote unaoanza kuona uhusiano wako unazama kwenye matatizo inabidi kuwa mkweli kwa kujiuliza swali mwenyewe "je hili ni kubwa zaidi kuliko vile ningeweza kufikiri ama kuomba?" Kama jibu ni hapana bass ujue kwamba Mungu amekuandalia mazuri mengi…. na ametuita tu watoto wake kufanya mambo mengi lakini maelewano yasiyofaa sio kati ya mambo mazuri kutoka kwa Mungu.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.