VIINGILIO TAMASHA LA PASAKA 5000

Na Mwandishi Wetu.

Kekeletso ndani ya tamasha la Pasaka mwaka 2014. Bofya hapa kuona picha.
Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2015 imetangaza kiingilio cha chini kwa wakubwa katika tamasha hilo litakalofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ni shilingi 5000.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati hiyo, Alex Msama kiingilio kwa watoto watakaojitokeza kwenye onesho hilo watalipa shilingi 2000.

Msama alisema VIP watachangia shilingi 10,000 na viti maalum watatoa shilingi 20,000.

Msama alisema kuwa ameamua kuweka kiingilio kidogo ili iwe rahisi hata kwa walio na uwezo mdogo waweze kuhudhuria tamasha hilo.

Tamasha hilo la mfano wake linalosubiriwa na wadau mbalimbali wa nyimbo za injili, litashirikisha wasanii mbalimbali wa nyimbo za injili ndani na nje ya Tanzania.

Aliwahakikishia usalama mashabiki wote wa muziki wa injili watakaojumuika kwenye tamasha hilo na kwamba usalama wa kutosha ambako alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi.

Kupitia Tamasha la Pasaka Mwenyekiti huyo anawapa pole wakazi wa Mkoa wa Iringa kwa ajali iliyotokea wili iliyopita iliyohusiaha basi la Kampuni ya Majinjah na lori la mizigo na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 43.

Ameongeza kuwa kupitia tamasha hilo anaendelea kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi (albanism) na kulaani vikali unyanyasaji huo.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.