WANAKWAYA WASALIMIKA KATIKA AJALI MBAYA YA GARI

Gari inavyoonekana baada ya ajali hiyoWaimbaji wa kwaya ya Uinjilisti Forest mkoani Mbeya walipatwa na ajali mbaya iliyohusisha gari la vyombo walilokuwemo pamoja na gari ndogo kwa kugongana uso kwa uso. Taarifa kamili ni kama ilivyotolewa na kwaya hiyo kupitia tovuti yake UINJILISTI FOREST

Tunafuraha kubwa kushirikiana nanyi katika kufurahia na kusifu UKUU wa Mungu wetu alie hai, kwa kuendelea kutushindia vita dhidi ya upinzani wa mwovu, ambaye kila kukicha anafanya kila aliwezalo ili kukwamisha na kuharibu kazi ya Mungu ya kupeleka injili ya YESU Kristo kwa watu na mataifa.

Tukio. Siku ya Jumamosi majira ya saa tatu usiku tulikuwa tukitokea kwenye huduma ya ndani toka kwa mmoja wa wapendwa wetu, tulikuwa tukirudisha vifaa vya muziki kanisani kwa ajili ya kuviandaa kwa ibada ya Jumapili. Tulipokuwa tunaingia barabara kuu, gari ndogo ilitokea kusikojulikana, na kujaribu kuyapita magari matatu kwa pamoja, bila kuangalia usalama wa magari mengine likiwepo la kwetu. Ghafla sana, dereva wetu hakupata hata muda wa kufanya lolote, tulijikuta uso kwa uso na hilo gari dogo. Waliokuwa kwenye gari letu ni Burton Mwakibinga, Isaya, Adam
Mungu ni mwema sana, maana hakuna aliejeruhiwa sana, dereva wetu alibanwa kwenye gari sababu ya uharibifu uliotokea, na kwa msaada wa wasamalia wema, tulifanikiwa kuvuta mlango, na kumtoa akiwa na jeraha mguuni. Alikimbizwa hospitali na kupata matibabu, na baadaye majira ya saa sita usiku wa Jumapili, aliruhusiwa kurudi nyumbani. Wakati huo huo kuna mwanakwaya mwenzetu Savina, nae alipatwa na ajali maeneo ya Soweto, siku hiyo hiyo ya Jumamosi jioni, lakini Mungu alimsimamia na kumlinda, amepata maumivu ya mbavu lakini anaendelea vema.

Picha ya gari hiyo wakati ikizinduliwa rasmi kanisani mwaka jana

Mungu alietoa chombo hiki, ndie ataketoa vingine kwa ajili ya kupeleka huduma yake mbele.

Tunaomba na kuwasihi wapendwa wote wenye mapenzi mema na kwaya ya Uinjilisti Forest pamoja na kazi ya Mungu, muendelee kutuombea na kuiombea kazi ya kupeleka injili ya YESU Kristo kwa watu wote, amaana mwovu shetani hafurahii wala kupenda kuona kazi hii ikifanikiwa na kusonga mbele, anafanya kila liwezekanano kuhakikisha kazi inarudi nyuma na kutukatisha tamaa.

Lakini Mungu wetu ni mwaminifu, na atatushindia vita hivi, na sisi tutaendelea kuifanya kazi yake tulioitiwa kwa ujasiri na ushujaa sababu jemedari wetu yupo na hatuachi kamwe kama tukiendelea kumtumikia kwa uaminifu.

Mwisho tunapenda kutoa pole kwa wote walioguswa na ajali hii kwa namna moja ama ingine, Mungu wetu wa mbingu aendelee kutupigania na kutupa faraja yake kuu ili kutoka hili pia, tujifunze na kushuhudia ukuu wake kwetu.
Baadhi ya waimbaji wa Uinjilisti Forest wakiwa katika huduma


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.