WANAWAKE WENYE UHITAJI KUSAIDIWA KIBIASHARA

Engineer Carlos Mkundi
Wanawake nchini wameshauriwa kubuni miradi ya maendeleo ili wajikwamue kiuchumi na kuepuka kuwa tegemezi kama ilivyo zoeleka kwenye jamii ya Kitanzania.

Wito huo umetolewa na rais wa taasisi ya Upendo kwa Mama, Engineer Carlos Mkundi wakati akizindua kampeni ya kuwasaidia wakinamama wenye uhitaji kupata vyanzo vya biashara.

Engineer Mkundi amebainisha kuwa mpango huo utakuwa unalenga zaidi kina mama wasiojiweza kimaisha kwa kuanzisha mashindano ili kinamama hao kueleza malengo yao na kisha kupata nafasi ya kusikika kwenye vyombo vya habari na kupigiwa kura na wasikilizaji.

Aidha rais huyo wa Upendo kwa Mama amebainisha kuwa mpango huo unaanza hivi karibuni kwa sababu taratibu zote zimesha kamilika.

Ametoa ufafanuzi wa jinsi ya kupeleka taarifa za mama aliye na uhitaji ili apate zawadi nono; kuwa unatuma ujumbe wa maandishi kwa simu ya mkononi kupitia namba 15522 ukianza na neno ONYESHA kisha jina la mama muhusika.

Baada ya kuwapata kinamama hao utaanza utaratibu wa kuwapigia kura kwa kusikiliza vipindi vya radio kwa kuwasikia wakieleza malengo yao.

Mbali na kinamama pia kuna shindano la kutunga wimbo bora unaowahusu kina mama ambapo washindi watapata zawadi nono.

“Ukitaka kushiriki kutunga wimbo unaohusu mama au ambao unao tayari unatuma jina lako kwenda namba 15522 ukianza na neno ONYESHA.”

Engeneer Mkundi amemalizia kwa kuwaomba wananchi kuwasaidia kina mama wanaohitaji kushiriki ili wapate mwanga na kipato cha kujikimu wao pamoja na familia zao.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.