WAPENDA MIUJIZA MAKANISANI, HII IMEWAPATA WENZENU

Hakika muyaonapo haya jua kwamba ule mwisho umekaribia… habari hii ya kusikitisha ni taa nyekundu kwa wakristo wote wanaotafuta miujiza ya watoto ama utajiri kwa kuhama hama makanisa yao kwa madai ya kutafuta neno la Mungu..

Picha ya mtandao ikionesha wanawake wajawazito, tukio tofauti na hili - lakini nchini Nigeria.
Huko nchini Nigeria wanawake zaidi ya 20 wakiwemo wake za watu na mabinti wamepachikwa mimba na "nabii" wao ambaye amedai aliambiwa na Roho mtakatifu kufanya nao mapenzi wanawake hao. Nabii huyo alifahamika kwa jina la Timothy Ngwu ambaye ni mchungaji kiongozi wa kanisa la Vineyard Ministry of the Holy Trinity huko Enugu tayari anashikiliwa na jeshi la polisi la jimbo hilo kwa kosa la kuwalazimisha kufanya nao mapenzi na wanawake hao.

Mchungaji huyo amedai anatii wito wake wa kinabii na kiroho alioitiwa na kufanya sawa na mapenzi ya Mungu kwa kuwapa mimba yeyote yule aliyechaguliwa na kuwekwa wazi na Roho mtakatifu bila kujali kama mwanamke huyo ameolewa ama la alisema msemaji wa jeshi la polisi Enegu kamanda Ebere Amaraizu akitoa taarifa kwa vyombo vya habari na kudai kwamba mwanamke akijifungua mtoto hubakia kwenye huduma hiyo na mzazi wake

Taarifa kutoka kwa familia za mchungaji huyo zinasema mkewe aitwaye Veronica Ngwu ambaye alichoshwa na tabia ya mumewe hasa alipompa ujauzito mdogo wake na kuamua kumripoti Polisi. Kwa upande wa kaka wa mtuhumiwa ambaye hakutaka jina lake lifahamike ameiambia Vanguard report kwamba amekuwa akimuonya kaka yake juu ya tabia yake kwa muda mrefu lakini hakutaka kusikiliza, amesema gadhabu ya Mungu imeshuka juu ya kaka yake.

"Ngoja niwaambie hasira ya Mungu imemshukia kaka yangu tumekuwa tukimuonya kila siku kuacha alichokuwa akifanya amejaza boma letu kwa kuzaa watoto bila uangalifu na kutuambia tunamuonea wivu kwasababu anafanya maagizo ya Mungu" alisema kaka mtu na kuongeza kwamba angalia majengo yote ya kanisa ameyageuza kuwa ya kwake kwa jina la huduma yake, alimfukuza mkewe wa ndoa waliyezaa naye watoto watatu na kuanza kuwajaza mimba wake za watu na mabinti wadogo, we angalia boma lote limejaa watoto wa jinsia zote alilalamika kaka huyo. 

Aidha kaka huyo amesema waumini wote wa kanisa la kaka yake ni wapumbavu kwasababu mwanamke hawezi kumuacha mumewe na kwenda na mwanaume mwingine kwa kisingizio cha kwenda kumuabudu Mungu na kufanya zinaa, na kudai hawezi kujiingiza katika tatizo hilo, "Vero amefungua msaada kwa wamama hao ngoja wayamalize na polisi ila nataka huduma hii ifungwe kabisa" alisema

Ngwu ameiambia NaiJ kwamba kaka yake ana wake wapatao watano na watoto 13 pamoja na wake za watu kwa madai ya kufuata mapenzi ya Mungu. Amedai hajawahi kufanya mapenzi na wake za watu ila amefanya hivyo endapo waume zao wamekubaliana na ombi la Roho mtakatifu. Calista Omeje na Assumpta Odo ni wanawake ambao waliawaacha waume zao ili kuishi na nabii huyo kwakuwa ilikuwa ni upako wa kinabii wa mchungaji huyo.

Calista ambaye ana watoto 10 na mumewe alipewa mimba na mchungaji huyo ila mtoto alikufa, amesema mwanamke huyo alimkabidhi mchungaji huyo binti yake huku Odo naye amesema mchungaji huyo amempa mimba yeye na binti yake.

Tofauti na nchini Nigeria, huko Afrika Kusini GK imewahi kuripotikuhusiana na dini ambayo waumini wake wanakula nyasi pamja na kukanyagwa migongoni, huku pia wakinywa petroli kwa madai kwamba ni juisi ya mananasi. Bofya hapa kusoma.

Nabii wa Afrika Kusini akikanyaga waumini kama sehemu ya mafundisho na maombi yake


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.