CHAGUO LA GK: KUNDI LA KUKUMBUKWA KWA KAZI YAO NJEMA TAMASHA LA PASAKA 2015 TAIFA


Chaguo la GK leo tunakupa dakika 12 za kuitazama kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama ya jijini Dar es salaam, jinsi ilivyobariki makumi elfu waliofurika katika uwanja wa Taifa kusherehekea kufufuka kwa Kristo wakati wa tamasha kubwa la kimataifa la Pasaka lililoandaliwa na kampuni ya Msama Promotions.

Kwaya ya Kijitonyama iliweza kunyanyua watu waliofika uwanjani hapo katika kumsifu Mungu, wakiimba kati ya nyimbo zao zilizowapa umaarufu ndani na nje ya nchi kama 'Hakuna Mwanaume kama Yesu, Simba wa Yuda pamoja na Hakuna Mungu kama wewe ambazo licha ya kwamba miaka imepita toka nyimbo hizo zitambe lakini kwa siku ya Pasaka zilikuwa kama ndio zinasikika kwa mara ya kwanza.

Ukiwahitaji Kijitonyama leo wapo ukumbi wa Makumbusho Posta ambao unatazamana na chuo cha usimamizi wa fedha cha IFM, watakuwa hapo kuwatia nguvu waimbaji wenzao wa Amkeni kutoka Kinondoni Lutheran ambao hii leo watakuwa wakirekodi live DVD wakisindikizwa pia na waimbaji wengine, tukio linaanza saa nane mchana kwa kiingilio cha shilingi 5,000 tu za Kitanzania. Mungu awabariki muwe na jumapili njema.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.