CHAGUO LA GK: NATAKA MAPATANO - MCH FAUSTIN MUNISHITwatumai umzima mdau wa Gospel Kitaa popote pale ulipo ulimwenguni. Chaguo letu kwa wiki hii linatoka kwa Mchungaji mwenye maskani yake nchini Kenya, Faustin Munishi.

Hivi karibuni Mchungaji Munishi alikuwepo kuhudumu kwenye tamasha la kimataifa la pasaka ambalo huandaliwa na kampuni ya Msama Promotions, ambapo aliimba wimbo; Nataka Mapatano. Wimbo ambao ulitungwa kwenda kinyume na wimbo wa marehemu Remmy Ongala, kifo hakina huruma.

Tunakutakia Jumapili yenye baraka huku tukikukumbsha kwamba ukipatana na BWANA Yesu, hutokuwa na haja ya kukiogopa kifo wala vichochezi vyake.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.