DAKIKA 25 ZA TAMASHA LA PASAKA ZILIVYONIBARIKI

Na Elie Chansa,
GK Staff Writer.

Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama
Kati ya matamasha ambayo hakika sijajutia kufika ni hili tamasha la pasaka, ambalo waandaji - kampuni ya Msama Promotions imetimiza miaka 15 kwenye kulifanya. Si tu kwamba maandalizi yalikuwa yalikuwa ya aina yake, lakini pia lilikusanya wahudumu kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Zambia amekuwepo Ephraim Sekeleti, Mchungaji Faustin Munishi (Mtanzania) ameletwa kutoka Kenya, Muimbaji Mnigeria (mwenye makazi yake Uingereza) amefika, bila kusahau malkia ya nyimbo za injili barani Afrika, Bi Rebecca Malope na Mchungaji Solly Mahlangu kutoka Afrika Kusini.

Hapa nchini wamekuwepo waimbaji kadha wa kadha. Wale waliozoeleka na hata wale ambao hawana mazoea. Yaani unahisi kabisa fulani akishika microphone nini kitatoea. Ila kuna wengine hujui nini kitafuata. Hapo ndipo dakika zangu 20 zinaingia. Dakika ambazo zimenifanya nisijute kusafiri masaa kumi na mbili kutoka Arusha. Kama bado sijaeleweka, basi nifafnue kwamba nazungumzia huduma ya kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama.

Uwepo wao kwenye tamasha hili umebadili kabisa taswira ya uimbaji uliozoeleka. Kwanza waliingia kwa style ya kipekee. Wachache wakatangulia jukwaani na kisha kuanzisha kabla wengine hawajaungana nao. Muziki uliopigwa live kwa ufasaha ukamaliza kabisa watu, na ukiongezea namna ambavyo walikuwa wanashambulia jukwaa kwa wingi wao - hakika hapo kila mtu aliyefika tamashani ana jambo la kuwazungumzia. Mungu awabariki mara dufu!

Dakika zao 12 jukwaani zilitosha kutuonjesha nyimbo zao tatu; Hakuna Mwanaume kama Yesu, Simba wa Yuda, na  Hakuna Mungu kama wewe. Kama isingekuwa kwa majukumu nyuma ya kamera, hakika ningekuwa bize kumchezea Mungu pamoja nao.  Nisiseme mengi. Ila waliofika uwanjani wanaweza kunisaidia.

Kwaya ya mkoa wa Mbeya miongoni mwa watu.

Kwaya ya Mkoa wa Mbeya pia ilibariki mno, wakongwe hawa na mvi zao na majukumu yao mengi, bado nguvu imo ya kumtumikia mungu. Step yao ya mikono ndo ikaniacha hoi kabisa. Hapa kama ulikuwa hujui, kwaya hii inaundwa na wachungaji na maaskofu. Kwa nyimbo zao mbili zao mbili walizoimba siku hiyo, hakika wachanga wamejifunza kitu. Kwa Mungu hakuna mkubwa wala mdogo, wote ni viungo vyake na yatipasa tutumike kwa kadri tuwezavyo.

Baada ya kuhudumiwa na hizi kwaya mbili, roho yangu ilikuwa imesuuzika, sikuwa na haja sana ya kumsubiri Rebecca ama Mchungaji Solly Mahlangu, ila kwa kuwa ilinipasa. Basi mwisho wa siku tutakuletea matukio kamili mwanzo mwisho.

Huyo ni mimi, sijui kwa wewe mwenzangu uliyefika, ulibarikiwa na nani hasa. Tuandikie maoni yako hapo chini.

Salamu kutoka Arusha.


Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.