HISTORIA KUANDIKWA JUMAPILI HII JIJINI DAR ES SALAAM,USIKOSE


Siku ya jumapili hii katika ukumbi wa Makumbusho ya taifa Posta mkabala na chuo cha fedha cha IFM jijini Dar es salaam, kunatarajiwa kufanyika tukio kubwa la aina yake wakati ambao kwaya ya Amkeni kutoka kanisa la Kilutheri Kinondoni itakaporekodi DVD live kwa mara ya kwanza na kwa viwango vya kimataifa.

Kwa mujibu wa mwalimu na kiongozi wa kwaya hiyo ndugu Dan Kullwa ambaye pia husifika kwa utunzi pamoja na upigaji wa kinanda kwa kiwango cha kimataifa, amesema kumekuwepo na msururu wa watu kurekodi live DVD siku za hivi karibuni kitu ambacho ni kizuri lakini jumapili hii itakuwa tofauti na namna watu walivyozoea kuona kwani siku hiyo kutakuwa na ladha tofauti ya waimbaji na vikundi vitakavyowasindikiza lakini pia mtiririko mzima ulivyopangwa pamoja na nyimbo zitakazorekodiwa zikiwa na lengo kuu la kumtukuza Mungu  "watu wakae mkao wa kupokea kitu cha tofauti ni mkao wa ibada yenye nyimbo za ladha mbalimbali!! Tutakuwa na kitu kinaitwa " high voltage praise and worship experience " Kullwa ameiambia GK"Watu Wategemee kukutana na Mungu hapo!! Pia hii ni first production ya audio na DVD ya jinsi yake!! Tunataka watu wapate vionjo vya tofauti na sasa inafanya kwaya, Pia tunafanya uimbaji huu wa next level Ku share na ulimwengu wa nyimbo za injili! Si kusikia tu Bali watu wapokee badiliko, Kwa gospel musicians wategemee vipindi vya kisasa kabisa vya worship na kusifu"

Aidha tulio hilo linakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 30 ya kwaya hiyo toka ilipoanza huduma yake katika usharika wa Kilutheri Kinondoni, ambapo kati ya waimbaji watakao wasindikiza Amkeni ni pamoja na Uinjilisti Kijitonyama, The Reapers kutoka Kimara, Uinjilisti Sayuni Kinondoni na waimbaji wengine. Kiingilio katika tukio hilo ni shilingi 5,000 na tukio linatarajiwa kuanza majira ya saa 9 alasiri.

Uinjilisti Kijitonyama ©MatukioMichuzi

Karibu, high voltage praise and worship

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.