KWA TAARIFA YAKO: MWIMBAJI ALIYEHAMA NA WIMBO WA KUNDI MAARUFU LA MUZIKI WA INJILI AFRIKA

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
KWA TAARIFA YAKO hii leo ni kukujulisha juu ya mwimbaji mmoja wa injili ambaye sauti yake ya kwanza imemfanya kuwa mmoja kati ya waimbaji wakutegemewa wa kundi maarufu la muziki wa injili barani Afrika la Soweto Gospel Choir kutoka pale nchini Afrika ya kusini. Mwimbaji huyu ambaye bado na kundi hilo akiwa mmoja wa waimbaji waanzilishi huwa anaambatana na kundi hilo kwa takribani ziara zote bara Ulaya, Asia bila kusahau Australia na Marekani ambako kundi hilo limekuwa likifanya ziara zake kila mwaka.

KWA TAARIFA YAKO mwimbaji ninayemzungumzia hapa ni mwanadada Sibongile Makgathe mwimbaji sauti ya kwanza wa kutegemewa wa Soweto lakini safari yake alianzia katika kundi la Joyous Celebration akiwa mmoja kati ya waimbaji wa kwanza wa kundi hilo ambalo kwasasa linazidi kushika kasi kwenye muziki wa injili nje na ndani ya bara la Afrika. Sibongile baada ya kuimbia Joyous na kuona imetosha kisha kujisajili wakati wa uanzishwaji wa Soweto Gospel Choir mwaka 2002.


Mwanamama Sibongile akiwa katika pozi

KWA TAARIFA YAKO mwanadada huyu alishiriki kurekodi na Joyous toleo la kwanza akianzisha wimbo maarufu wa tenzi uitwao Joko Ea hao wimbo ambao aliuimba kwa ustadi na kuweza kufika ufunguo wa juu kabisa katika kuanzisha, haijajulikana ni kwanini alipojiunga Soweto Gospel Choir akapewa kuanzisha tena wimbo huo huo ambao waliurekodi kwa mara ya kwanza kwenye live DVD rekodi yao nchini Australia, hata hivyo licha ya kuimba kwa ustadi wimbo huo, hali haikuwa nzuri pale alipojaribu kupanda ili aimbe kwa sauti ya juu kabisa ambapo sauti iligoma, na kwakuwa ilikuwa live basi ikawa vigumu hata kufuta kile kilichofanyika.
Sipo akiwa na Sibongile

KWA TAARIFA YAKO Sibongile ambaye safari yake ya uimbaji alianzia toka mwaka 1989 lakini mafanikio ni mara baada ya kuanza na Joyous kisha Soweto alipo, anajulikana pia na waimbaji wakubwa wa muziki wa ndani na nje ya kanisa kama wakina Sibongile Khumalo, amefanya ziara na mwimbaji maarufu ambaye kwasasa marehemu Michael Jackson, ameimba na mwanamama Angelique Kidjo bila kumsahau mwanamama Miriam Makeba ambaye kwasasa ni marehemu.

KWA TAARIFA YAKO Sibongile ni mwanadada mpole na ambaye kwa muonekano haonyeshi kuwa na majivuno na kipaji alichopewa na Mungu, hata GK ilipopata kukutana naye jijini London mwaka juzi wakati kundi hilo lilipokuwa ziarani hakusita kusalimiana na GK na kuahidi kuongea naye mengi zaidi tukijaaliwa.


Ambwene akiwa pamoja na Sibongile jijini London mwaka juzi.Hiyo ndiyo KWA TAARIFA YAKO kwa leo, vinginevyo tukutane wiki ijayo….
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.