KWA TAARIFA YAKO : NABII ALIYESEMA ANGEFUFUKA BAADA YA KIFO CHAKE, ALIPATA PIGO NIGERIA

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
KWA TAARIFA YAKO leo tupo kwa upande wa manabii ambao wameendelea kutikisa sehemu mbalimbali za dunia kwa tabiri zao ama miujiza ambayo huifanya na kufanya watu wengine kusema kwamba nguvu za giza zinahusika katika miujiza yao. Wiki hii tulikuandikia ushuhuda kuhusu mwanadada kutoka Sierra Leon aliyewakuta watu maarufu kuzimu kama hukusoma BONYEZA HAPA, na kati ya watu hao maarufu ni aliyekuwa nabii wa kanisa maarufu nchini Sierra Leon liitwalo Burning Busha Ministry Frank Emmanuel Tamba Mani kwa jina maarufu Papa ambaye naye alikutwa na dada huyo akiwa kuzimu.

KWA TAARIFA YAKO nabii huyu ambaye alifariki dunia na umri wa miaka 34 katika uhai wake
Marehemu Nabii Mani
alifanikiwa kuwa na majina mazito yote ya utumishi kama mchungaji, askofu, nabii na kadhalika. Mchungaji huyu alifariki dunia katika hospitali ya kijeshi iliyopo Freetown nchini kwake lakini aliahidi kwamba angefufuka baada ya siku tatu na kuagiza watu wasiuzike mwili wake ili kujionea alichokisema. Lakini kabla ya kifo chake mchungaji huyu aliugua kwa takribani mwaka mmoja huku wengi wakidhani tayari alishakufa katika kipindi hicho cha ugonjwa.


KWA TAARIFA YAKO nabii huyu alikuwa maarufu sana nchini kwake hasa kwa miujiza aliyokuwa akiitenda kama kuponya magonjwa yaliyoshindikana, ukimwi, vipofu kuona, viwete kutembea bila kusahau kuwatoa watu katika vifungo mbalimbali vya kimapepo kama wachungaji na manabii wengine wanavyofanya nchini na kwingineko barani Afrika na duniani kwa ujumla ingawa huyu uvumi ulikuwa umeenea kwamba anatumia nguvu za giza kutenda hayo yote.

KWA TAARIFA YAKO mchungaji huyu inadaiwa aliwahi kufariki mara ya kwanza lakini akafufuka tena na kuahidi akifa mara ya pili atarudi akiwa na nguvu za ajabu kupamabana na shida na karaha za dunia hii, ingawa kwa bahati mbaya akafariki kimoja mpaka leo. Mmoja kati ya waumini waliowahi kupata huduma kanisani kwa nabii huyo ameliambia jarida moja la mtanadaoni la nchini humo kwamba wafanyabiashara maarufu, viongozi wa kisiasa na watu wa aina zote walikuwa wakimiminika kwa nabii huyo kupata huduma. October mwaka 2008 alipoanza kuumwa nabii Mani aliandika kitabu chenye jina "Forty-five Minutes at the Grave" ama dakika 45 kaburini, kitabu ambacho aliandika juu ya ufahamu wake kaburini na maisha ya kaburini kwa ujumla pamoja na maswali aliyowahi kuwauliza kaburini ndugu na rafiki zake waliokufa alipokutana nao kaburini.

KWA TAARIFA YAKO toka alipofariki mchungaji huyo mwezi October 26, 2009 hajafufuka mpaka leo, huku ikielezwa kwamba chanzo cha kifo chake inawezekana ikawa mambo hayakwenda vizuri alipokwenda nchini Nigeria kuongeza nguvu za giza ambako inadaiwa alikuwa akichukua nguvu hizo ambazo hata hivyo alikuwa akipewa kwa muda na zinapokaribia kuisha alitakiwa aende tena kupewa upya na ndipo inadaiwa aliporejea alianza kuumwa mpaka umauti kumpata.na ndipo huyo dada aliyepata wasaa wa kupelekwa kuzimu na kurejea amesema alikutana na nabii huyo akiwa kuzimu.

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO hii leo, kikubwa kuwa makini na umuombe sana Mungu kuhusu mahali uliposimama kama ni kweli ni Mungu mwenyewe atendaye ama ni nguvu za giza. tukutane wiki ijayo...


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.