KWA TAARIFA YAKO: VITUKO VYA IMANI YA WACHEZAJI MPIRA WANAPOKUWA UWANJANI

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Mganga na kanga wake. ©Biyokulule
Kwenye tasnia ya mpira wa miguu, kuna mengi huwa yanaendelea na pia kuwa maarufu miongoni mwa mashabiki. Mojawapo ni lile linaloitwa "kusafisha nyota", ambapo baadhi ya wachezaji wa soka na huenda kwa waganga wa kienyeji, ili ama kujihaikishia nafasi vikosi, vya taifa hata vilabu vyao. Ni tambia mbaya sana, lakini huonekana kama jambo la kawaida zama hizi.

Pamoja na uwepo wa watu wa namna hiyo, hapo ndipo bado utagundua kwamba wale wanamtegemea Mungu bado pia wao kwenye kila sekta. Hapa KWA TAARIFA YAKO anayezungumziwa ni kiungo wa klabu ya Everton ya nchini Uingereza, Steven Pienaar. Muafrika Kusini huyu anafahamika na wenzake kikosini kwa kuwa na tabia ya kuomba Mungu kila mara wanapotaka kuingia uwanjani, jambo ambalo humtofautisha na wale wazee wa ndumba.

Steven Pienaar ©Reuters
Sanjari nayo, jambo ambalo Pienaar hupendelea kufanya ni kusikiliza nyimbo za injili, pindi ambapo wanakuwa safarini na hakuna kinachoweza kufanyika kuachilia mbali story za hapa na pale pamoja na wenzie.

KWA TAARIFA YAKO jambo hili limekuwa la kipekee kwa kuwa kuna wachezaji wengine barani Ulaya ambao huwa wanavaa soksi nje ndani ama hata kwa kugeuza bukta zao za ndani kutokana na maelekezo ambayo wamepewa na "wataalamu" wao. Mmoja ya watu ni John Terry, ambaye amekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza na Chelsea the Blues, ambaye yeye hakai siti nyingine zaidi ya ileile kwenye basi la klabu, hawezi kupaki gari mahala popote zaidi ya eneo moja tu, hufunga kamba za viatu kwa vifundo vitatu, na pia imani nyingine nyingi tu za kushangaza.

kipa Iker Cassilas ©Marca
Iker Cassilas, golikipa wa muda mrefu wa Real Madrid yeye huvaa soksi nje ndani tokea msimu wa mwaka 2008/09 kabla ya kuacha zoezi hilo mwaka 2012 mara baada ya kocha Mourinho kumtupa benchi, jambo ambalo halikuwa hi kutokea kwa kipindi cha miaka 10.

Nje ndani ©Getty images
Gonzalo Higuain ambaye anachezea klabu ya Napoli kwa sasa, yeye huwa na tabia ya kukanyaga dimba kwa mguu wa kushoto kwanza na kisha kupiga hatua tatu kabla ya kugusa chini ni na kiuchora ishara ya msalaba.

Paul Ince kipindi akiwa Manchester United, alikuwa mara zote ni mtu wa mwisho kuingia uwanjani, lakini pia KWA TAARIFA YAKO daima alikuwa akivaa jezi yake pale anakaribia kabisa kuiacha korido inayounganisha vyumba vya kubadilishia nguo na dimba.


Paolo Di Canio yeye mara zote bila hata kusahau, alikuwa akivaa kwanza kiatu cha mguu wa kushoto kisha kufuatia na cha upande wa kulia, hakuna siku alibadili tokea aanze kufanya hivyo.

Pelé ©Myhero
Imani za namna hii ziko nyingi kwenye michezo duniani, ambapo KWA TAARIFA YAKO gwiji wa soka duniani, Edson Arantes do Nascimento Pelé kuifuatilia jezi aliyogawa kwa mshabiki, mara baada ya kuona kiwango chake kimepungua mno. Alichokifanya Pelé  ni kumuagiza rafiki yake wa karibu afuatilie ile jezi iliekea wapi, ambapo mara baada ya kurudishiwa, gwiji huyo alirejea kakika kiwango chake cha kawaida. KWA TAARIFA YAKO jambo ambalo hakujua ni kwamba rafiki yake huyo alimtafutia tu jezi nyingine mpya na kumuambia kuwa ndo ile aliyoigawa.

KWA TAARIFA YAKO hayo ndiyo machache kati ya mengi yanayojiri viwanjani. Vinginevyo tukutane wiki ijayo.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.