LOVE SONGS TO JESUS IJUMAA HII KKKT MBEZI BEACH


Ijumaa hii macho yote yapo kwenye Night of Worship with Saxaphone. HIi ni mara ya kwanza Tanzania nzima na hata Afrika kwa ujumla. Hapo tunazungumzia Love songs to Jesus Ijumaa tarehe 10 Aprili 2015 ndani ya K.K.K.T Mbezi Beach kuanzia saa mbili usiku hadi kunakucha.

Wito wa kujifunza Saxophone umekuja hasa baada ya kujua kwamba saxophone ni 'romantic instrument', kwa ajili ya 'love songs'. ndipo hapo Roho Makatifu akasema na Mise juu ya kuabudu kwa njia ya Saxophone, maana kama upendo upo kwa binadamu, Mungu je itakuwaje hapo.. Anaeleza Mise wakati akihojiwa na GK. Imezoeleka Mise kuwa peke yake, ila siku hiyo wapo wapiga Sax 4 tofauti (Njoo umuone G Sax, njoo umuone Mosax). Mbali na hao pia kutakuwa na wahudumu wengine kama vile John Lisu, Bomby Johnson, Upendo Kilahiro na Miriam Mauki pamoja na wengineo wengi, bila kusahau Mbezi Beach Praise Team.

Tukio hili ambalo liko prepaid na BWANA Yesu, hakuna haja ya kuja na kiingilio, ni bure kabisa ambapo kutakuwa na masaa mawili ya kumuabudu Mungu. Lakini haya yote yataambatana na inspirational talks, comedy, Neno la Mungu, na hata maombi ya kizalendo kwa ajili ya taifa kwenye kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu. 

Kama unasikitika kwamba inafanyika Dar es Salaam, basi ni kwamba kura zilipigwa na hatimaye kura zikaanguia Dar es Salaam, kati ya miji mingine ikiwemo Mbeya, Mwanza na Arusha.

Saxaphone pekee inatosha kuabudisha, piano pekee inatosha kuabudisha, kusoma Zaburi pekee kunatosha kuabudisha. Huku ndiko tunakoelekea. Kumuabudu Mungu katika hatua nyingine ya juu.

Fire TV, Kiango TV, Word Alive Streaming TV na Agape TV zitakuwepo kurusha hili tukio live moja kwa moja.

Yote kwa yote, usalama upo wa kutosha.

Kama hujafahamu bado kinachozungumziwa, jaribu kutazama video zifuatazo. Ama bofya hapa.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.