MAMA WA MIAKA 76 AKUTANISHWA NA BINTIYE MIAKA 49 TOKA ALIPOJIFUNGUA AKIAMBIWA ALIFARIKI

Mama na mwana wakiwa wenye furaha baada ya miaka 49 toka watenganishwe
Hebu fikiria unapoambiwa kitu katika moja ya siku yako kubwa maishani, siku ambayo mtoto wako alizaliwa lakini alifariki mara baada ya kuzaliwa ….lakini unakuja kugundua mtoto wako yupo mahali fulani duniani. Hiki ndicho kilichotokea kwa mwanamke huyu wa huko Missouri nchini Marekani.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 76 anayefahamika kwajina la Zella Jackson Price kutoka eneo la Olivette Missouri ameishi nusu ya maisha yake akiamini binti yake alifariki siku alipomzaa. Lakini mwanamke huyo alipatwa na mshtuko alipogundua kuwa amekuwa akiishi akimini uongo alioambiwa kwa miaka 49 alipojifungua binti yake na kudanganywa kuwa amefariki. Binti yake anayefahamika kwa jina la Melanie ambaye ni mzima wa afya hatimaye aliweza kukutanishwa na mama yake mzazi, binti huyo aliyekuwa ameasiliwa na familia nyingine alitaka kumjua mama yake mzazi toka siku nyingi na alipatwa na mshituko ndoto yake ilipotimia kwakukutana na mama yake mzazi pamoja na kaka yake

Melanie amemshukuru Mungu kwa nafasi ya pili kuweza kukutana na mtu aliyekuwa anamuhitaji kwa muda mrefu sana, ingawa binti huyo ni kiziwi lakini anaweza kujieleza kwakutumia lugha ya vitendo. Mungu ni mkubwa. Hata hivyo haijaelezwa ilikuwaje mwanamama huyo kuambiwa mtoto wake amekufa kumbe alichukuliwa na familia nyingine. Ambapo kwa mujibu wa taarifa, familia hiyo inapanga kuanza uchunguzi wake kujua nini kilitokea hospitalini kwa mtoto huyo kuchukuliwa.

Angalia video mama na bintiye walipokutanishwa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 49


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.