MAMBO MACHACHE YANAYOATHIRI AKILI YAKO

Na Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.©Clker

1. HISIA/MISISIMUKO (EMOTIONS).

Hisia/Misismuko zilizopo kwenye mwili wa binadamu ni aina ya kemikali amabazo zinazalishwa kwenye mwil kwa sababu mbali mbalii.Kimekali zinapoamshwa ndipo hisia/misisimuko huamka.Akili ndio yenye uwezo wa kuamua Hisia zimaake au hapana.Hisia/Misismuko za mwili zinapaswa kuwapo kwa kiwango fulani na zinapaswa kuwa zinatawaliwa na akili yako ili kuweza kuzielekeza kitu kipaswacho kufanya.Hisia/Misisimuko ni Kama Mto wa Maji, Na Akili ni Mithili ya Mkondo wa Maji.Maji yasipowekewa Mkondo basi husambaa bila sababu za msingi na matokeo yake hupelekea kuleta madhara mbali mbali kwa jamii.Hali kadhaliki akili ambayo hutawaliwa na kuendeshwa na misisimuko?Hisia ambayo haijadhibitiwa hupelekea akili kuweza kufanya kazi kwa kiwango cha chini.Hali ya Misisimuko/Hisia ambazo hazidhibitiwa kwa usahihi huwa na adhari kwa muhusika .Mfano Hasira zisizokuwa na Msingi,Chuki,Huzuni.Ni Muhimu kuangalia namna uvyodili na misisimuko kwenye akilia yako.Hakikisha hauwi Mtumwa Misisimuko/Hisia bali Wewe unakuwa kiongozi mwema wa misisimuko/hisia zako.


2. MSONGO WA MAWAZO( STRESS).

Akili ya mwanadamu ni moja ya sehemu muhimu kwenye maisha kwenye kufanya maamuzi mbalimbali kwenye kila jambo linalomuhusi yeye binafsi.Msongo wa Mawazo ni mlindikano wa vitu mbali mbali kwenye akili yako.Kuna wakati akili inakuwa na mambo mbalimbali.Kwa Muda wa Siku Moja  ubongo huwaza mawazo mawazo 65000-90000 lakini mawazo yanafanyiwa kazi na akili ni machache sana.Akili inapokuwa na mlundikano wa mambo mengi kwa wakati mmoja inashindwa kuchuja na kufanya kazi kwa usahihi.Msongo wa Mawazo hufanya akili kuchanganyikiwa na kushindwa nini cha kufanya kwa wakati mmoja matokeo yake kuna kuwa na mambo mengi ambayo huyawezi kufanywa kwa ufanisi.Ni Muhimu kuhakikisha unapunguza  Msongo wa Mawazo.Mlundikano wa Mawazo lazima uwe na kiasi na unapozidi lazima athari za moja kwa moja kwa muhusika huonekana,yawezeka ikawa ni afya lakini athari kubwa zaidi huanza kwenye akili na pindi akili inaposhindwa kufanya kazi kwa ufasa matokeo ya maamuzi huwa ya mabaya nay a kusuasua


3. HABARI UNAZOSOMA KILA SIKU(INFORMATIONS).

Mara nyingi tunasikia msemo Habari ni Nguvu,Mtu anapokuwa na habari za kutosha maana yake ndipo anakuwa n nguvu za kutosha.Hali Kadhali akili,Habari unazosoma kila siku kwenye maisha yako zinawezakuathiri akili zako na namna ya utendaji wako.Unapotumia muda mrefu kusoma habari zisizokuwa na msingi na maana ni kama kuweka Mbegu ya magugu kwenye shamba,Unapoweka magugu kwenye shamba maana yake magugu hayo yatasababibisha mimie ya maana kufa na kubakiwa na magugu.Fikiri iwapo mtu tangu anazaliwa anapendikiziwa magugu ya Chuki kwenye Akili yake, Je Unafikiri  itakuwaje? Habari njema na nzuri nai afya kwa akili yako na itakusaidia kuweza kuboresha utendaji wako wa kila siku na kuongeza ufanisi kwenye mambo kadha wa kadha.Hakikisha hausomi,hausikilizi,Hautazami,Hauandiki habari zisizokuwa na amsingi mara zote maana kufanya vivyo haumuathiri mtu mwingine unajiathiri wewe mwnenyewe.Madhara yanaweza yasionekane sasa lakini kuna wakati yatajionyesha tu.


4. KUMBUKUMBU MBAYA ZILIZOPITA (PAST BAD EXPERIENCES).

Akili iliyojuruhiwa ni zaidi ya ugonjwa wa kawaida,Kumbu za majeraha yaliopitia yalipelekea kuathiri utendaji wako wa kili siku usipojifunza kuyadhibiti mara nyingi huwa na athari kwa sehemu kubwa kwenye akili yako.Kumbu Kumbu mbaya husababishwa kuzalishwa kwa  misisimuko/hisia(emotions)  katika kiwango cha juu  matokeo yake hisia hizo zilizo zidi akili hushindwa kuzidhibiti na hupelekea kuathiri akili zako na utendaji wako.Kumbu kumbu mbaya ni mithili ya mtu aliyefungwa kitambaa kwenye macho alafu anaambiwa vuka barabara yenye magari yaendayo kasi.Ni nguvu kuvuka haraka maana itaepelekea yeye kupata ajali ambayo itamepelekea mauti.Hakikisha akili yako haijawi na kumbukumbu mbaya zilizopita maana zinaathiri kwa sehemu kubwa utendaji wako wa akili.
___
E-mail:naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless Y’All


Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.