MAMBO MATANO AMBAYO KILA MTU HUPENDA KUFANYIWA

Na Faraja Mndeme,
GK Contributor.

1.KUSIKILIZWA.
Moja ya hitaji muhimu la mwanadamu yoyote ni kupenda kusikilizwa na watu wanaomzunguka.Hakuna mwanadamu yoyote ambaye hapendi kusikilizwa.Unapompa  mwingine thamani ya kumsikiliza unapata nafasi ya kuweza kupata nafasi kwenye moyo wake.Hata iwapo muda mwingine huenda kinachoongelewa hakikupendi sana,msikilize bila kumuhukumu wala kumwingilie pindi anapozungumza.Msikilize kwa umakini na utaratibu.Mara nyingi huenda tunasikiliza ili kuweza kutoa majibu ya kile kinachozungumzwa lakini muda mwingine imetupasa kusiliza tu bila kutoa jibu lolote.Baadhi wengine hawajawahi kupata nafasi kusikilizwa bila kuhukumiwa na wengine hawajawahi kusikilizwa kabisa.Hii ni Moja ya namna mojawapo ya kuweza kupata kibali kutoka kwa wengine.

2. KUPENDWA.
K wa miaka kadha wa kadha sijawahi  kutana na mwanadamu ambaye anasema hapendi kupendwa.Kila mmoja wetu wanatamani kuona hisia zao zinathaminiwa.Kupenda mwingine kuna ambata na mambo kadha wa kadha.Unapoaamua kuwapenda wengene hauangali namna walivyo na n wanaweza kuwa na mchango gani kwenye maisha yako bali unapojenga utamaduni wa kuwapenda wengine unapata wigo mpana wa kuweza kupata kibali kwenye maisha yao binafsi,biashara,kazi na kwenye shughuli mbali mbali.Ni muhimu kuhakikisha unawapenda wengine bila ukomo.Upendo hauchagui,umri,rangi,kabila au dini.Upendo ni lugha inayoweza kuongelewa na mioyo yote ya wanadamu ulimwenginu.Wapende wengine bila kuhukumu namna ya makosa yao yalivyo na madhaifu yao.


3.  KUTHAMINIWA.
Kila mmoja wetu anatamani kuonekana ni bora kwa wengine licha ya madhaifu walio nayo.Mahangaiko mrngi tunayoyaona leo kwenye ulimwengu huu ni ya kutafuta kuonekana una aina fulani ya thamani.Mavazi tunayovaa,vyakula tunavyokula,makazi yetu na mambo mengi haya yote yanaonyesha namna kila mtu anavyopenda kuonekana ni bora hata iwapo kuna mapungufu kadha wa kadha.Thamani ya mwanadamu haishuki bali tabia ya mtu ndio inaweza kushuka au kupanda thamani.Thamani ya mwanadamu haina kilinganisho cha gharama hapa ulimwenguni.Hakikisha unajenga utaratibu wa kuwathamini wengine,thamini mawazo yao,maisha yao na kile wanachokifanya bila kujenga hali ya kutanguliza kuhukumu bila kuonyesha uthamani wao.


4. KUKUBALIWA.
Wanadamu wengi wa dunia ya tatu tumekuwa na chgamoto ya kuwaku bali wengine kama walivyo,Mahangaiko mengi tunayoyaona leo ni kwa sababu wengi wetu hatujajengewa mfumo wa kujikubali na kuwakubali wengine kama walivyo.Madhaifu yao ndio nguvu zetu,Ni muhimi unajenga kuwakubali wengine bila kujenga hoja zisizo na msingi ambazo zitaonyesha wa kuwadhalilisha na kuwafedhehesha.Muda mwingine iwapo unaona huwezi kumkubali mtu kama alivyo usionyesha kitendo chochote ambacho kitaonyesha hisi hasi ambazo zitakuwa hazina msingi wowote.Unapotaka kibali kwa moyo wa mwingine anza kumkubali na kupokea kama alivyo.Taratibu taratibu ndipo unaweza kumsaidia kutokana na hali aliyokuwa nayo.


5. KUPONGEZWA.
Miezi michahche iliyopita nilikuwa nafanya kozi fupi ya namna ya kuwafundisha Mbwa ili kuweza kufanya kile unachotaka.Katikati ya kozi niligundu moja ya hatua muhimu ya pale Mbwa anapofanya vizuri kile ulichomwagiza basi Unampongeza.Mara unapojenga utamaduni wa kumpongeza ndipo alipojenga jitihada za kufanya vyema zaidi kili ulichomwagiza afanye.Je iwapo Mbwa napenda kupongezwa vipi kuhusu mwanadamu ambaye ana hisia kamili? Ni muhimu unajenga tabia ya kuwapongeza wengine pale wanapofanya vyema bila kinyongo na kijicho.Wapongeze na wafurahie kwa mafanikio yao.Pongeze zinaweza zisiwe vitu vya thamani  bali hata namna unavyowazungumzia kwa wengine.Kuna njia kadha wa kadha ya kuonyesha pongezi zako kwa wengine.Pongezi ni moja ya njia nyingine ya kupata kibali kwa Wakuu na Wanadamu pia.


E-mail:naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless Y’All
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.