MAMIA YA WAUMINI WA KANISA LA GWAJIMA WAFURIKA NYUMBANI KWAKE BAADA YA TAARIFA ZA POLISI KUMZINGIRAMamia ya waumini wa kanisa la Ufufuo na Uzima nchini lililochini ya Askofu Josephat Gwajima walikusanyika nyumbani kwa kiongozi wao huyo maeneo ya Salasala jijini Dar es salaam, mda mfupi uliopita baada ya kuwepo taarifa za jeshi la polisi likiwa na silaha za moto pamoja na magari wakiwa wameizingira nyumba hiyo huku taarifa hasa za kuhusu uvamizi huo zikiwa hazijajulikana bado.

Mda mchache uliopita mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo ametoa taarifa kupitia ukurasa wa Facebook wa kanisa hilo kuwajulisha waumini kwamba baada ya jeshi hilo kufika nyumbani kwa mchungaji huyo toka majira ya saa kumi za alfajiri hawakufanikiwa kuingia ndani kwakuwa uzio wa nyumba ya mchungaji huyo imewekewa umeme hivyo baada ya kuwepo takribani masaa kadhaa taarifa hiyo inadai askari hao wameondoka eneo la tukio mda mfupi uliopita na kumpa mwanya mchungaji huyo akiwa na wasaidizi wake kuondoka kwa maana ya sasahivi kuelekea polisi ili kuwauliza uwepo wao nyumbani kwake siku yaleo.

KUHUSU KILICHOTOKEA NYUMBANI KWA ASKOFU GWAJIMA LEO.
Polisi wamefika nyumbani kwa askofu Gwajima mnamo majira ya saa kumi usiku, na walikua wakijaribu kuruka ukuta, lakini walionekana kushindwa na mmoja wao alisikika akitoa taarifa ya kuwa wameshindwa kuruka kwasababu ya electric fance..alisikika jirani mmoja akiongea..
Mnamo alfajiri kulikua na mvua kidogo ambapo watoto wa askofu huyo walionekana wakitoka kwenda shule kwenye gari aina ya wish. Na majira ya saa kumi na mbili ...na nusu mvua ilipokatika gari ilirudi ndani na mara, Polisi walipovamia na kuanza kugonga mlango kwa nguvu wakitaka kufunguliwa.
Polisi hao mwanzoni walikua wamevalia kiraia kabisa hivyo hawakufahamika kama ni polisi kweli au La.
Kuna vijana watatu waliokua wakipita eneo hilo. Walikamatwa na kupigwa makofi na kuhojiwa kama ni wa kwa Gwajima.
Tofauti na taarifa zilizosambazwa na clouds fm kuwa askofu huyo alikataa kuwafungulia baada ya wao kujitambulisha SI ZA KWELI, maana taarifa za uhakika kutoka kwa majirani polisi hawakufunguliwa mlango kabisa.
Polisi walikuja na magari mengi huku wakitaka kuingia ndani kinyume na sheria. Ambapo waliwaza kuruka na kushindwa kutokana na fance iliyopo.
Taarifa za jeshi la polisi kwa waandishi si za kweli.
Askofu Gwajima ameelekea central polisi kwa sasa bila escort ya polisi, akienda kusikiliza walichomjia asubuhi kwa magari na silaha za moto.
Updates will flow...
See More

 

Magari ya polisi yakiwa nje ya nyumba ya Askofu Gwajima maeneo ya Salasala jijini Dar es salaam.

 
 
Umati wa waumini wakiwa wamejitokeza baada ya polisi kuondoka. Picha zote mali ya Ufufuo Crew
 

Wakati huohuo, kwa mujibu wa taarifa mpasuko kutoka kituo cha ITV zinasema Askofu Gwajima amefikishwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam. Taarifa zaidi utazipata kadri tutakavyozipata
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.