MASHAMBULIZI CHUO KIKUU GARISSA


Alhamisi, tarehe 2. Nikiwa mpakani Namanga kutokea Nairobi Kenya, nakutana na taarifa ya TV ambayo inaonyesha kwamba Chuo Kikuu cha Garissa kiko kwenye mashambulizi. Habari hiyo ambayo ninaipata mida ya saa nne asubuhi inanistua sana, ambapo kumbukumbu za mashambulizi ya Westgate yaliyotokea Septemba mwaka 2013 iliyoripotiwa kuchukua uhai wa watu 67. Soma hapa.

Ni taarifa za kusikitisha ambazo mwisho wa siku ikaelezwa kwamba watu 147 wamefariki dunia. Na hapa sizungumzii tu familia zaidi ya 150 ambazo ziko kwenye kilio. Lah, hili ni jambo la Kenya nzima, na hata Afrika Mashariki kwa ujumla. Achilia mbali dunia nzima ambayo inafuatilia kwa masikitiko tukio hilo ambalo liliripotiwa kumalizika jana baada ya mpambano kati ya jeshi la polisi wakishirikiana na jeshi la ulinzi la Kenya.

Ilivyotokea
Alfajiri ya Alhamisi, mida ya saa kumi na moja, njozi za watu zikiendelea usinginzini, huku wengine wakiwa kwenye maombi yao ya asubuhi, ndipo ghafla watu wanaoripotiwa kuwa wanne waliingia na kuanza kushambulia mabwenini huku wakihoji nani muislamu, na nani siye - ili kulenga shabaha zao vema. Limekuwa shambulizi la kigaidi kutoka kikundi cha Al-Shabaab (kama walivyodai wenyewe).

Miili ya wasomi hawa ambao ni tegemeo kwa taifa la Kenya na dunia nzima kwa ujumla ilikuwa imetapakaa, wengine wakiwa na matundu ya risasi visogoni, ikionesha namna ambavyo walikuwa wanajaribu kujihami aidha kwa kulala chini ama kwa kukimbia popote pale katika juhudi za kujinusuru.


"Tulichambua watu na kuwaachia Waislamu. Kuna miili ya Wakristo wengi waliokufa humo ndani. Pia tunawashikilia mateka wengi wa Kikristo. Mapigano yanaendelea humo ndani." Ananukuliwa Sheikh Abdiasis Abu Musab wa Al Shabab


Tayari wizara ya mambo ya ndani imetangaza dau la shilingi milioni 20 kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kaw Mohamed Mohamud almaarufu kama Dulyadin, ama kwa jina lingine Gamadhere, kwa kuhusika na shambulizi hilo.

Japhet Malwa yeye kwa upande wake siku ilianza hivi. "Tulikuwa tumelala pale tuliposikia mlipuko wa bomu, na kisha risasi zikaanza kurindima. Kila mmoja wetu alikimbia kujaribu kujinusuru." Anaieleza Agence France-Press (AFP)

Kuna ambao hawakuweza kukimbia mara moja na hivyo kukutwa na magaidi ambao waliwaua. Nina bahati kuwa hai kwa maana niliruka fensi pamoja na 

Kwa upande wake Collin Wetangula anasema yeye alikuwa anajiandaa kwenda kuoga na ndipo ghafla akasikia milio ya risasi kutoka Bweni la Tana. Iliwabidi wajifungie pamoja na wenzake 4 kwenye chumba chao. Kwenye korido walisikia sauti za watu wakikimbia kimya kimya kuhofia kwamba iwapo sauti zitatoka basi wangejulikana walipo.

Sauti ngeni ya washambuliaji ilisikika vema ikisema "sisi ni Al-shabab" kwa Kiswahili fasaha, lafudhi ya pwani. Associated Press imeelezwa.

Cha muhimu kwa muda huu, ni kuendelea kuliombea taifa la Kenya wapate amani ya BWANA Yesu na hatimaye kuendelela na majukumu yao kama kawaida. Kenya si tu sehemu ya Afrika Mashariki, bali pia ni ndugu zetu. Jina la BWANA lihimidiwe.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.