PICHA ZA MATUKIO DUNIANI KWA WIKI ILIYOISHA JANA

©Jorist Wise
Ndani ya siku moja kuna mengi yanaweza kutokea, lakini katika wiki moja, matukio ya kutisha yameikumba dunia, ambapo vifo na majeruhi wengi yametokea. Kuanzia huko Chile ambapo kumekuwa na mlipuko wa Volcano Calbuco uliohamisha maelfu ya wakazi nchini humo, hadi Nepal ambapo zaidi ya wananchi 3500 wanahisiwa kufariki dunia, huku zaidi ya wengine 6000 wakijeruhiwa. Kuachana na hilo, Kaskazini mwa bara la Afrika, majanga ya melei kuzama yanazidi kutokea ambapo wahamiaji wamekuwa wakijaribu kuvuka bahari ili kusaka maisha bora barani Ulaya, Italia ikiwa ni nchi ya kupitia.

Zifuatazo ni picha za matukio hayo kama ambavyo GK imekukusanyia.

Chile

Takriban wakazi 1500 wamehamishwa makazi yao kutokana na mlipuko wa volcano Calbuco ambayo, ambayo imelipuka baada ya miaka 42. madhara makubwa yamejitokeza kusini mwa nchi hiyo, ikiwemo miji ya Puerto Varras na Puerto Montt ambapo maeneo kadhaa yamefunikwa na majivu, jambo ambalo lieleta taharuki kwa binadamu na mifugo.
Mlipuko wa volcano ulioambatana na majivu na radi. ©David Cortes Serey/AFP
Taswira kabla ya mlipuko © Andeshandbook.org
Taswira kutoka upande mwingine. ©Martin Bernetti/AFP/Getty images
Majivu yaliyotokana na mlipuko huo, ambayo pia huathiri usafiri wa anga kwa kiasi kikubwa. ©AP Photo/Diego Main/Aton Chile
Vijana wakiondoa majivu kwenye paa la nyumba yao, ambayo yametokana na mlipuko wa volcano. ©Martin Bernetti/AFP/Getty images
 
Mji ukiwa umebadilishwa rangi kwa uwepo wa majivu ya volcano Calbuco. ©EPA/Felipe Trueba
Armenia
Takriban miaka 100 iliyopita kwenye vita kuu ya kwanza ya dunia (1914-1918), kulitokea mauaji ya takribani Waarmenia milioni moja na laki mbili, ambao walishambuliwa na majeshi ya utawala wa Ottoman (Uturuki). Hata hivyo taifa la Uturuki limekataa kkubali kwamba mauaji hayo yalikuwa ya halaiki. Wakati Armenia wanaadhimisha kwa masikitiko, Uturuki kwa upande wao watakuwa wanaadhimishwa kwa shangwe.

Hivi karibuni Papa Francis alinukuliwa akiyaelezea mauaji hayo kuwa ya halaiki, jambo ambalo lilizua tafrani baina ya taifa la Uturuki na Vatican. Mataifa kadhaa ikiwemo Ufaransa na Urusi yameainisha mauaji hayo kama ya kimbari. Ujerumani imekuwa taifa jingine ambalo hivi karibuni limetoa rai kwa mauaji hayo kutambulika kama ya kimbari. Marekani haiyatambui mauaji hayo kama ya kimbari.

Sehemu ya waombolezaji kwenye kumbukumbu ya miaka 100 ya mauaji ya kimbari nchini Armenia
Mtazamaji akitazama picha kwenye makumbusho ya mauaji ya halaiki nchini Armenia. © Karen Minasyan AFP/Getty Images.
Sehemu ya waandamanaji nchini Armenia, tarehe 24 Aprili 2015.

Burundi
Nchini Burundi kwake Rais Pièrre Nkurunziza machafuko yamezuka na kupekelea vifo vya watu watatu, mara baada ya chama tawala nchini humo, CNDD FDD kutangaza kuwa  Rais Nkurunziza atagombea kwa awamu ya tatu kiti hicho, taarifa ambayo iliibua mtafaruku baina ya vyama vya upinzani vya siasa sanjari na wananchi.

Kufuatia hali ya hofu iliyotawala nchini humo, tayari wakimbizi wanaokadiriwa kuwa zaidi ya laki moja wameshavuka mpaka na kukimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na Uganda - ambapo Tanzania nayo  inatarajiwa kupokea.

Polisi wakitawanya wananchi kwa virungu na gesi "mabomu" ya machozi. Kwa nyakati nbyingize, silaha za moto zimeripotiwa kutumika. ©Reuters

Polisi wakikabiliana na wananchi. ©AFP
Nepal
Tetemeko la ardhi ambalo limeikumba Nepal limepelekea zaidi ya wananchi 3,700 kufariki dunia na wengine zaidi ya 6,000 kujeruhiwa, huku Umoja wa Mataifa ukikadiria kwamba watoto zaidi ya milioni 1 wanahitaji makazi, kutokana na madhara yaliyojitokeza.

Taifa hilo ambalo limebarikiwa kuwa na milima mirefu duninani imeshuhudiwa na mataifa mengine ikipeleka wanajeshi 9 kati ya 10 katika zoezi la uokoaji, ambapo pia mataifa kama Marekani, Ujerumani, Israel, na India wamepeleka misaada na vikosi vya uokoaji, ili kunusuru madhara zaidi ya yale ambayo yamekwisharipotiwa tayari.

Licha ya majengo kuporomoka, majeruhi kadhaa pia wameripotiwa kutoka Mlima mrefu zaidi duniani, Everest, ambapo tetemeko lilipelekea barafu kufunika watalii na waongozaji wao. Tetemeko hilo limeripotiwa kuwa na kipimo cha richa 7.9

Sehemu ya kivutio cha utalii ikiwa imebomolewa na tetemeko hilo
Zoezi la uokoaji likiendelea.
Wanajeshi kazini
Wakazi wakijaribu kumuokoa mtu aliyefunikwa na kifusi ©Narendra Shrestha/EPA
Manusura wa tetemeko hilo akitolewa na waokoaji. ©Omar Havana/Getty Images

Mabaki ya makazi yaliyoharibiwa na tetemeko, Kashamandu, Nepal ©Navesh Chitrakar/Reuters
Athari upande wa barabara. ©Xinhua/Zuma Press
Manusura wa tetemeko akiwa amejawa na hisia ©Narendra Shrestha/EPA
Mwili wa mkazi wa Kashmandu ukiwa umefunikwa na kifusi. ©Navesh Chitrakar/Reuters
Kama unaishi kwa amani, basi hauna budi kumshukuru Mungu licha ya makwazo mengi unayokutana nayo. Sanjari na hilo, usiache kuombea majanga yaliyotokea kwa wananchi wa mataifa haya (wenzetu). Tukutane wiki ijayo.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.