MATUKIO YA KWAYA ZETU NCHINI WAKATI WA SIKUKUU YA PASAKA

Hizi ni baadhi ya picha tulizozipata za matukio ya baadhi ya kwaya zetu nchini ambazo zilishiriki ibada za Ijumaa Kuu mpaka kufufuka kwa Yesu Kristo ama sikukuu ya Pasaka. Kuna kwaya zilizosafari kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine na pia kuna zile zilizoshiriki sikukuu hiyo katika sharika zao.

Kwakuanza ni kwaya kongwe nchini ya Tumaini Shangilieni kutoka Arusha wenyewe siku ya Ijumaa Kuu walitoa huduma katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini humo ambako kulikuwa na ibada ya pamoja kwa makanisa ya jiji hilo kama ilivyo ada yao kwa makanisa hayo kufanya ibada ya pamoja kila mwaka.

Kwaya ya Uinjilisti Foresti kutoka kanisa la Kilutheri Foresti jijini Mbeya wenyewe walikuwa kwenye mwaliko wa kihuduma huko usharika wa Kilutheri wa Kana uliopo mjini Tanga, ambapo watumishi hao waliweza kutoa huduma usharikani hapo pamoja na wenyeji wao.
Picha za chini pia ni kutoka kwaya kongwe ya Uvuke, inayopatikana kanisa kuu la Anglicana makao makuu ya nchi mjini Dododma, kwa upande wao walitoa huduma ya uimbaji kanisani kwao, wakiwa wamependeza na sare zao mpya nadhifu kama waonekanavyochini.

Picha chini, ni kwaya maarufu nchini ya AIC Chang'ombe (CVC) wao walikuwa na mwaliko katika kanisa la AIC(T) Bwiru jijini Mwanza, ambako walishiriki kuanzia Ijumaa Kuu mpaka pasaka, sambamba na kuwasindikiza waimbaji wenzao wa TCRC katika uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.Picha za chini ni kwaya nyingine maarufu ya Uinjilisti Kijitonyama, kwa uapnde wao wenyewe walisherehekea sikukuu ya Pasaka usharikani kwao Kijitonyama Lutheran kisha mchana wa Pasaka walikuwa na mwaliko wa tamasha la Pasaka katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam lililoandaliwa na kampuni ya Msama Promotions kwa mujibu wa wahudhuriaji wanasema Kijitonyama waliweza kuonyesha makali yao katika kumsifu Mungu na kubariki wengi.
Ukiachana na Uinjilisti Kijitonyama, kwa upande wa wadogo zao kwaya ya Vijana Kijitonyama wenyewe walikuwa kwenye huduma huko mkoani Arusha katika usharika wa Kilutheri Kijenge, ambapo licha ya kushiriki katika ibada kanisani hapo, pia kwaya hiyo ilipata nafasi ya kuhudumu kwenye mkutano wa Umoja wa wanafunzi wa Kikristo nchini mkoani Arusha (UKWATA) mkutano ambao ulifanyika katika shule ya sekondari ya Enaboishu. Ukiachana na tukio hilo pia kwaya hii ilipata wasaa wa kutembelea kituo cha watoto yatima na kuwapatia zawadi mbalimbali. Huduma yao ilikuwa njema sana hadi kufikia kualikwa nyumbani kwa mmoja wa waumini wa Kijenge ili kupata chakula cha mchana ikiwa pamoja na kuimba naye.


Tukio lingine ni kwaya ya Neema Gospel kutoka kanisa la AIC(T) Chang'ombe jijini Dar es salaam, kwa upande wao Ijumaa Kuu walishiriki ibada kanisani kwao kisha mchana saa 9 walishiriki ibada iliyoandaliwa na jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) katika usharika wa AIC (T) Magomeni jijini humo. Jumatatu ya Pasaka kwaya hii ilikuwa VCCT kwa mchungaji Huruma Nkone. Tumebahatika kupata picha moja tu


Picha zote ni mali za kwaya husika. Tutakupa wasaa wakutazama picha zote za tamasha la Pasaka kutoka uwanja wa Taifa, endelea kusubiri.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.