MSAMA PROMOTIONS YATOA MISAADA KWA YATIMA


Katika kuelekea sikukuu ya pasaka, kampuni ya Msama Promotions imetoa vyakula mbalimbali ikiwemo unga, mchele, mafuta, na mbuzi lengo ikiwa ni kuwasaidia watoto yatima na watu waishio katika mazingira magumu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, mkurugenzi mtendaji wa Msama Promotions, Bwana Alex Msama ameeleza sababu na madhumuni ya kutoa msaada huo uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 6 kuwa ni ili kusheherekea pamoja na wasiojiweza, kama ambavyo Biblia inaeleza kuhusu dini iliyo bora.

Nao baadhi ya watoto wa vituo mbalimbali wakipokea msaada huo kwa sura ya tabasamu wakinona nao ni watoto kama watoto wengine wanaosoma.

Kampuni ya Msama Promotion huwa kila mwaka wanatoa msaada kwa watoto yatima ni waishio katika mazingira magumu lengo wajisikie nao ni kama binadamu na ni wetu kama wengine.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.