NENO LA LEO - ALHAMISI

NENO LA LEO
"Itakuwa kabla hawajaomba nitajibu, wakiwa katika kusema nitasikia" (Isaya 65:24).

Mambo ya kujifunza:

1. Mungu hajawahi kuchoshwa na maombi ya watu.

Mungu anataka kujibu maombi yako kuliko wewe unavyopenda kumwomba.
(Mathayo 7:7-10).

Mungu anataka kutatua shida, changamoto, majaribu na magumu unayopitia kuliko hata wewe unavyotamani kuvushwa.
(Zaburi 91:14-16).

Mungu hafurahii hali nzito na ngumu unazopitia na anataka ashiriki kuzitatua na kukupa furaha iliyopotea.
(Yoh 16:23-24).

Mungu ameweka maombi kama njia pekee ya kuuleta Ufalme wa mbinguni kwenye changamoto, magumu na hali tunazopitia.
(Mathayo 6:9-12).

Kadri unavyokuwa na kiwango cha kukutosha cha Neno la Mungu (Mapenzi yake kuhusu jambo unaloliombea), ndivyo unavyokuwa na uhakika wa kupata kile alichosema na kuahidi kwako.
(Yohana 15:7, 1Yoh 5:13-14).

Mungu anataka kugeuza maisha yako kuliko wewe unavyotamani ageuze maisha yako.
(Isaya 43:18-19, Ayubu 14:7-9).

2. Majibu ya maombi yako huwa yanatolewa tangu muda ule unapoamua kwa dhati kumtafuta Mungu japo inaweza kuchukua muda kiasi kuonekana mwilini.
"Kabla hawajaomba nitajibu"

Danieli alijibiwa tangu siku ya kwanza japo majibu yalifika siku ya Ishirini na moja (Danieli 10).

Yabezi alijibiwa na Mungu siku ileile aliyomwendea Mungu ili abadilishe maisha yake, japo mabadiliko yalikuja kuonekana baada ya muda kiasi (1Nyakati 4:9-10).

Mungu aliyajibu maombi ya Hana tangu alipotamkiwa Neno na kuhani Eli lakini ilichukua karibu mwaka mzima kumpata Samweli (1Samweli 1).

Linapokuja swala la maombi, usitie shaka.
Mungu wa Bwana wetu Yesu bado anajibu maombi.
"Mkumbushe, mhojiane, mueleze mambo yako akupe haki zako" (Isaya 43:26).
"Umuombe naye atakupa" (Zaburi 2:8).

NB: Hakikisha umesoma maandiko haya yote na kuyatafakari ili kuzalisha imani ndani yako.

Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.