SOMO: FAIDA ZA KUTEMBEA KATIKA BARAKA ZA AGANO NA MUNGU (3 & 4) - MWALIMU MWAKASEGE

Mwalimu Christopher Mwakasege

Kama hukusoma sehemu ya kwanza na yapili ya somo hili wiki iliyopita basi BONYEZA HAPA kabla hujaendelea na sehemu ya 3 na 4. Barikiwa

SEMINA YA MWL MWAKASEGE DODOMA

SOMO: FAIDA ZA KUTEMBEA KATIKA BARAKA ZA AGANO NA MUNGU.

Neno kuu: Eph 1:3


DAY THREE.
Utangulizi: Jambo ambalo Yesu alitaka tulikumbuke tunaposhiriki chakula cha Bwana ni agano jipya, pia faida ya baraka ndani ya agano hilo. Ebr 8:6
•Ndani ya ahadi kuna baraka za Bwana, baraka ni matokeo ya agano.
•Baraka zilizopo ndani ya agano ndizo zinazofanya ukristo uwe mtamu kuliko kitu chochote.
•Baraka zingekuwa zinafanana( nje na ndani) ya agano kusingekuwa na maana/ umuhimu wa agano.

MISINGI MINNE MIKUBWA YA BARAKA ZA AGANO.

1.Mungu kujijulisha au kujitambulisha kwa mwanadamu ya kuwa yeye ni Mungu na kuwa hakuna kama yeye. Ayubu 22:21-25, Yoh 10:10, 17:1-3,6. 2Pet 3:18

Mjue sana Mungu uwe na amani.

•Huwezi kumtumikia Mungu vizuri na kufanikiwa bila kumjua yeye.

2. Kurudisha mahusiano yaliyokuwepo kati ya Mungu na mwanadamu kabla dhambi haijaingia na tutengeneza uhusiano mpya. Eph 2:10-13,21-22

•Mungu anarudisha mahusiano yaliyopotea. Anatutengeneza tuwe maskani yake katika roho.


3. Kurudisha mfumo wa ufalme wa mbinguni hapa ulimwenguni ili uwe ndio mfumo wa maisha ya mwanadamu. Math 6:33, 4:17

•Tubu maana yake ni kubadilisha mtazamo wako wa kifikra. Lazima ujue mfumo wa ufalme wa Mungu. Math 6:9-10

•Mapenzi ya Mungu hutimizwa ndani ya ufalme wa Mungu kama haupo ni vigumu kutimiza mapenzi ya Mungu.


4. Ushiriki na uwajibikaji wa mhusika katika agano husika. Ebr 8:9-10

•Hakuna agano bila wahusika.

•Unapoingia katika agano ingia na nyumba yako. Kumb 28:1-14.

•Huwezi kukaa katika agano na kuwajibika katika nafasi yako na baraka za Mungu zikakupita.

•Ndani ya agano wewe mwenyewe ni baraka.


DAY FOUR.


Utangulizi: Gal 3:13-14 Tumebarikiwa kwa baraka zote.

•Zote maana yake zaweza hesabika/ zimehesabika.

•Swali: wewe umebarikiwa na baraka ngapi? Una baraka ngapi za Ibrahim ambazo zimekufikia? Luk 22:19-20, Ebr 8:6

•Huwezi kutenganisha baraka za Bwana na agano lake. Mwa 17:18-21, Luk 22:14-15.

•Agano: ni uamuzi unaolenga kujenga mahusiano ya kudumu baina ya pande zisizopungua mbili.


MAAGANO 7 MAKUBWA AMBAYO MUNGU ALIFUNGA NA MTU.


1.Agano la Nuhu. Mwa 6:18

2.Agano la Ibrahim. Mwa 15:18

3. Agano la Sinai ( Musa). Kut 19:5-6, Yer 34:12-13.

4. Agano la Daudi. Yer 33:20-21.

5. Agano la Lawi ( agano la chumvi). Hes 18:19, 2Nya 13:5

6. Agano la Yerusalem. Eze 16:1-62

7. Agano jipya ( Agano la Yeremia). Yer 31:31.


VIPENGELE MUHIMU KATIKA AGANO

1. Agano.

•Ni uamuzi wa Mungu kufanya agano na wanadamu ili kufanya mahusiano mapya na wanadamu.

•Agano linamfanya Mungu kumkubali mwanadamu

•Dhambi inafanya mwanadamu kutengana na Mungu.

2. Thabiti. Mwa 6:18

3. Kuthibitisha agano. Mwa 9:8-11

4. Ishara ya agano. Mwa 9:12.

5. Afanyalo. Mwa 9:12

6. Nitalikumbuka agano/ kukumbuka agano. Mwa 9:14-16.

7. Nililoliweka. Mwa 9:17.

8. Kiapo. Ebr 6:13-20


VIPENGELE MUHIMU VYA KUTUNZA MAHUSIANO YAKO NA MUNGU

1. Kiapo

Maana yake ni kifungo cha nafsi ya yule aliyeapa kufanya alichosema ayafanya.

Amu 2:1, Eze 16:8, Zab 89:35, Hes 30:1-2

2. Kuthibitisha.

Somo litaendelea…..

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.