SOMO: UHUSIANO WA VITI VYA ENZI NA MAFANIKIO YAKO (6 & 7) - MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE

Karibu katika mwendelezo wa dondoo za somo la Uhusiano wa viti vya enzi na mafanikio yako kama lilivyofundishwa na mwalimu Christopher Mwakasege mapema mwezi March mwaka huu katika Viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam. Kama hukubahatika kusoma sehemu zilizopita basi BONYEZA HAPA. kama ulishasoma, endelea na somo hili hapa chini kwa sehemu ya 6 na 7. Barikiwa
Mwalimu : Christopher  Mwakasege
Siku ya 6 ya semina viwanja vya Jangwani Dar es salaam.


Mambo Muhimu yakuyajua tunapozumgumzia juu ya kiti cha enzi


Ufunuo 13:2,7

<1>Shetani huwa anatumia kiti cha enzi kuwatawala watu na makundi yao

Mat 23:1,2

Shetani huwa anatumia mtu aidha katika kabila,taifa,lugha au kanisa nk na kumpa nguvu zake ili apigane na waatakatifu wote na kutengeneza mfumo ambao utafanya utendaji kazi wake uwe wa urahisi


<2>Kanisa linatakiwa kutumia kiti cha enzi cha kristo ili kushinda vita na shetani

Efeso 2:6

Efeso1:17-24

Efeso 6:10-12
Kanisa la efeso lisingeweza kufanikiwa kama lisingekaa katika kiti cha enzi na kristo Yesu

Ufunuo 5:9,10

<@>Kiti cha enzi na madhabahu vinaenda pamoja

Mungu alilisimisha kanisa la efeso na akalipa nguvu na kiti cha enzi na mamlaka na kutengeneza mfumo ambao utafanya kazi ya Mungu iende kwa urahis


<3>Pamoja na kiti cha enzi kuwepo ili kuwasaidia watu wake bado kuna uwezekano wa wale walio wake kushindwa kukaa katika kiti hichoUfunuo 3:21

Kanisa la waadokia lilishindwa kuketi kwenye kiti cha enzi na sio kwamba lilikataa kuketi,na kwakushindwa kwao kuketi kanisa lilikua likiishi chini ya viwango na shetani alikua anatumia kiti chake kuwashambulia


<4>Unaketije kwenye kiti cha enzi ulichopewa au unaketije kwenye nafasi ambayo Mungu ameweka katka ulimwengu wa Roho?

Jibu :Unaketi kwa ishara ya imani ambayo inaonyesha umekubali mambo mawili yafuatayo

1.Nafasi

2.Agano lililotengeneza iyo nafasi

Zab 89:3,4,20

Yeremia 33;20,21

Kol 1:16


Kumbuka ; viti vinatambulika kwa majina(mfano ;kiti cha Musa,kiti cha Daudi....),au vinatambulika kimajukumu (mfano ;kiti cha Hukumu,Kiti cha Rehema)

Musa alipotengenezewa kiti alikataa kwanza,Yeremia nae alipotengenezewa kiti alikataa kwanza,pia Ester alipotengenezewa kiti alikataa kwanza

Je unakubalije kiti cha enzi?

Ili ukubali kiti upate kuketi ni lazima uingie katka maombi ya kukubali kuonyesha kwamba umekubali

Ester 4:12-17

Ester aliwaambiwa akina mordekai waombe kabla haja sign ile nafasi yakupewa kiti

Ester 5:1

Ester alipovaa mavazi alionyesha tayari yuko katka ofic na alionyesha tayari kaket katka kiti cha enzi


<5>Utajuaje kama umeketi?

Ufunuo 3:21

Ishara ambazo zitakusaidia kujua kwamba umeketi

(A):Angalia kibali ulichonacho kutoka katka viongoz wa ngazi yako(ktk ulimwengu wa Roho ukipewa kiti kina eneo lake na ngazi yake ya kumiliki)

Ukipewa kiti na ukiket ni lazima upewe heshima na kibali kwa watu wanaokuzunguka au unaowaongoza,kinyume na hapo

ni kwamba umeket katka kiti ambacho haujakikubali katka ulimwengu wa Roho

Ester 5:1-2

Mfano:Angalia vijana katka makundi yao ni nani mwenye mamlaka na ushawish,huyo huwavuta vijana wenzake wengi kuj upande wake

(B)Jinsi ambavyo Mungu anakupa kujua namna yakupigana na icho kiti kinachopingana na ww

Ester 2:..,(mordekai alikua akikaaa au akiketi katika lango..)

Mordekai alipata ufahamu na kujua hayo mambo na vita alivyokua akipambana navyo vinawinda kiti cha ester kwasab alikua amekaa kweny kiti


(C)Angalia utiiisho wa Mungu unaokuzunguka unao ambatana na sauti ya mamlaka unaoambatana na kuzaliwa kwa maadui ambao hukututarajia

Uko upako wa mtu anayekaa katka kiti na kutumika mbele za Bwana

Kama umeshindwa kuketi kitu gani kimekushinda na kukufanya usiketi?

Ufunuo 3:21

Kama Yesu alishinda na yy anataka ushinde

Je alishinda katka nn na wapi?

Efeso 2:6

Mamlaka ya Yesu aliyokua nayo baada ya kufufuka ni ya tofauti na ni ya juu sana kuliko kipindi kile alichokua akiishi kabla hajafa

Yesu alipewa kuketi baada ya kushinda

Alishinda katka lipi?

Kuna mahali alisema ktk biblia

==Roho i radhi lakini mwili u dhaifu......(Vita ya kimwili)

==Roho yangu inahuzuni kiasi cha kufa.......(vita ya kiroho


Waebrania 12:2SOMO: UHUSIANO WA VITI VYA ENZI NA MAFANIKIO YAKO

SIKU YA SABA


Nataka nikukumbushe mambo manne ya muhimu kufahamu:

1. Shetani anaweza kutumia kiti chake cha enzi kama silaha mojawapo ya kukupiga vita mtakatifu

Ufunuo 13:2,7

2. Maana ya kiti cha enzi

Kiti cha enzi maana yake ni Nafasi iliyopo katika ulimwengu wa roho na ina mamlaka juu ya maisha na mwelekeo wa maisha ya watu katika eneo

3. Kila aliyeokoka anayo nafasi na anao uhalali wa kuketi na Yesu kwenye kiti chake cha enzi

Waefeso 2:6

Waefeso 1:21

Ufunuo 5:9,10

4. Ili uwe na mamlakaya kutumia nafasi uliyopewa na Yesu ni lazima uketi

Ufunuo 3:21

Mfano: kama we mwanamke, na unafanya kazi ofisini, na pia una pia una biashara, na pia unafanya kazi kanisani.

Maana yake una nafasi nne unazotakiwa kukaa kwenye kiti. Nyumba na maeneo yake, ofisini, biashara, na kanisani.

Ukikaa kwenye kiti maeneo yote hayo unakuwa na mamlaka maeneo yote hayo.

Kumbuka huwezi kuwa na mamlaka bila kuketi

Ukiketi kwenye kiti katika kila nafasi uliyonayo unakuwa na mamlaka kila eneo.

Nakwambia shetani atapata shida sana. Kwa sababu kila akienda anakuta eneo linamilikiwa tayari.

Akienda ofisini anakuta imeuzwa, nyumbani anakuta pameuzwa, shamba limeuzwa, nk vyote vinauzwa kwa damu ya Yesu. Lakini hii inakuja baada ya kuketi

Hatua nne za kufanya ili kupambana na viti vya enzi vya shetani.

1. Hakikisha umeketi pamoja na kristo

Maana hakikisha umekubali kutumika kwa ajili ya ufalme wa Mungu

Ufunuo 3:21

Unafikiri kwa nini shetani anaogopa wakristo wengi wakae kwenye kiti cha enzi?

Ngoja nikuoneshe siri iliyoko kwenye kiti cha enzi.

Ufunuo 3:21,22

Ufunuo 4: 1-11

Pia soma

Ezekiel 10:1

Ufunuo 5:11-14

Isaya 6:1,2,3

Kwenye kiti cha enzi kuna haya yafuatayo:

* chini kuna makerubi

* juu kuna maserafi

* kimezungwa na malaika wengi sana,

* kuna Roho saba wapo pale

* kimezungukwa na upinde wa mvua

* kwenye kiti kuna umeme na sauti na ngurumo


Sasa unaweza kuelewa kwa nini shetani hztaki wakristo wakalie viti vya enzi.

Ukikubali kuketi kila kinachosemwa katika kiti cha enzi kinahusu. Kwa sababu unaketi pamoja na kristo.

2. Jifunike damu ya Yesu ikulinde, wewe pamoja na lile eneo ambalo unapambana nalo.

Mathayo 23:1,2

Kutoka 11:4,5

Mungu hakumruhusu Musa aende kwa Farao pasipo kiti.

Waebrania 11:28

Kwa imani Musa akamchinja Pasaka.

Sababu ya Musa kupaka damu kwenye nyumba zao ni:

• pigo kutoka kwa Mungu lisiwapate wao

• shetani atakapokuja na hasira asiweze kuwapiga

Unapoenda kufanya vita na kiti lazima uhakikishe umeyafunika kwa damu ya Yesu mambo yako

Hakikisha unalinda nyumba yako, imani yako, mwili wako, biashara yako, kazi yako, uhai wako, mafundisho unayopata, mzaliwa wako wa kwanza nk kufuatana na vita unayopigana.

Unaachilia ulinzi wa damu ya Yesu. Ukiachilia damu ya Yesu shetani hawezi kufanikiwa hapo maana anaifahamu damu ya Yesu.

3. Omba toba kwa ajili ya kile kilichosababisha kiti kikapata nafasi na kikapata mtu wa kukikalia na kukitumia


Ufunuo 2:12-16

Zaburi 89:3,4

Kumbuka kiti cha enzi hakiji hewani ama ni cha Mungu au cha shetani

Kiti cha enzi kinafungwa katika agano kwa lazima utubu ili kuondoa uhalali wa hicho kiti.

4. Omba Mungu ahukumu juu ya miungu inayotumia kiti hicho

Hesabu 33:4

Kutoka 12:12

Kupigwa kwa wazaliwa wa kwanza Misri Mungu alikuwa anahukumu juu ya miungu ya kimisri

Zaburi 89:14

Misingi ya kiti cha enzi cha Mungu ni:

I. Haki

II. Hukumu


Kumbuka:

- ukiwa na madhabahu peke yake

Maana yake una nguvu lakini huna mamlaka kisheria


- Ukiwa na kiti peke yake

Maana yake una mamlaka lakini hauna nguvu.


Madhabahu na kiti huenda pamoja.


Ndo maana ktk ufunuo 13:2 utaona joka yaani shetani anampa mnyama nguvu, nk

Kwanini? Shetani anajua kuna agano kwa hiyo anampa nguvu mnyama. Ndo maana ukianza kupambana na viti vya enzi utaona upande wa giza saa ingine wakitumia wanyama kama paka, nyoka nk

Hukumu

Maana yake tenganisha nipate kuadhibu


Takasa

Maana yake tenganisha nipate kutumia.


Kwa hiyo omba Mungu mwenyewe ahukumu.

Hii ni siri ya ajabu unahitaji kufahamu!


Tutamalizia wiki ijayo… Mbarikiwe

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.