SOMO: UHUSIANO WA VITI VYA ENZI NA MAFANIKO YAKO (sehemu ya mwisho) - MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE

Karibu katika sehemu ya mwisho wa dondoo za somo la Uhusiano wa viti vya enzi na mafanikio yako kama lilivyofundishwa na mwalimu Christopher Mwakasege mapema mwezi March mwaka huu katika Viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam. Kama hukubahatika kusoma sehemu zilizopita basi BONYEZA HAPA kama ulishasoma, endelea na sehemu ya mwisho.Siku ya Nane

Ufunuo 13: 2 na 7: "Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi" Kazi mojawapo aliyopewa yule Joka (joka anasimama badala ya shetani" Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.* Mwaka jana tulijifunza siku 3, sikutegemea Mungu angenipa kulifundisha tena Dar es asalaa, na kuna somo nililokuwa nimelianandaa na roho mtakatifu akanikatazaREVIEW SUMMARY

1. Shetani anaweza kutumia viti vya enzi ktk kuwapiga vita watakatifu na si kila mtu, ingawa wengine wanaweza jikuta ktk vita isiyowahusu.....kuwa ktk ya vita hainamaana kwamba inakuhusu

2. Vita hii ni kwa watakatifu, watu waliotengwa kwa ajili ya kusudi la Mungu...utakatifu ni kutengwa kwa ajili ya kusudi la Bwana....hata vitu vya weza takaswa kwa ajili ya kusudi....Hata asieokoka anaweza kuwa mtakatifu maana kama viti, meza vya weza takaswa kwa ajili ya kusudi la Mungu si zaidi sana mwanadamu.....Ukisimamia kusudi la Mungu shetani atakupopiga vita...unaweza kuta mtu ambaye si mkristo anasimamia kweli au haki na kupigwa vita, hapigwi vita kwa ajili ya dini yake bali ni kwa ajili ya kusimamia kudusi la Mungu.....Na watu wa aina hii ni rahisi Mungu anawatembelea

3. Kiti cha enzi ni nafasi ktk ulimwengu wa roho...nafasi ya kimamlaka inayotengenezwa au na Mungu au shetani..... nafasi hiyo inatumiwa na miungu kwa kutumia watu walio kwenye hizo nafasi......


Neno mwenyekiti ni la kiroho kabla halijatumika mwilini...mkiwa watu wa tano na kupewa kazi kisha mmefika sehemu ya mkutano mkachangua mwenyekiti hii haina maana wengine wamekosa kiti, bali mtakyemchagua atakuwa na mamlaka kwa sababu ya nafasi.....4. Efeso 2: 6 ..Tumefufuliwa na kuketisha na kristo juu sana...hii inamaana baada ya kuokoka unaweza keti na kristo juu sana...Efeso 1:20-21..juu sana kuliko falme, mamlaka....kama umeketi pamoja na kristo umepewa nafasi....ufunuo 5:.. Yesu amekununua na kukufanya uwe mflme na kunani na kumiliki juu ya nchi......Ili uwe na mamlaka lazima uketi yaani ukubali hiyo nafasi ili Mungu aitumie hiyo nafasi kwa jili yake....Fanyeni yote kwa utukufu wake...ukipewa hiyo nafasi tafuta utukufu wa alikupa....wale wa kambi nyingine wakipewa kiti wanafanya matakwa ya joka la sivyo wanaondolewa kwenye hiyo nafasi....Kumbuka kama ni kiongozi mahali basi hiyo nafasi si kwa ajili yako ni ya aliyokuweka na unaowangoza...ukisha weka ubinasfi unakuwa mzigo kwa unaowatumikia na unakuwa mzigo kwa waliokuweka.......
Kwenye maandiko pia unapopewa nafasi si kwa ajili yako....Lazima ukubali kutumia hiyo nafsi kwa ajili ya ukufu wa Bwana.....

5. Si kila mapambano au shida imetokana na kiti cha enzi...yapo mampambano yaliyokuja ambayo yametokea kwenye mamlaka ambayo wakristo wameshindwa.....ukishafahamu vita yako ni ya viti baadaa ya kupima unahitaji msaada wa kiti...huwezi pigana na kiti bila ya kwenda na wewe na kiti na ukashinda.....hii ni neema ya ajabu, maana isingekuwa rahisi kwa kila mtu kuachiliwa kujifunza sasa.....Mungu ameruhusu somo la namna hii ni ili ujue kuna msimu mwingine na ili ujua kujipanga

6. Jana tulijifunza hatua 4 ukishajua unapambana na kiti, ...yaani ukiona mapambano mfano ukoo unakubana...kamani ni kanisani ukishaona kikao na wazee wa kanisa..ukishaona maswa yako badala ya kushughulikiwa na mtu yanapelejkwa kwenye kikao ujue ni kiti.Hatua nne:

1. Hakikisha umeketi...kuna kiti unatakiwa uketi..


Musa hukuruhu siwa kwenda vitani kwa farao bila kiti maana nguvu za farao zilikuwa kwenye kiti cha mzaliwa wa kwanza na Musa alikataa ndipo Mungu akampa haruni kuchukua kiti......Ilimchukua Ester maombi ya siku 3 ili aketi


2. Hakikisha unajifunika na damu ya Yesu ikulinde wewe na wanaokuzunguka....Mungu alimwambia Musa kile kiti cha enzi cha farao, farao hajakaa bali mzaliwa wa kwanza hivyo nitapiga mzaliwa wa kwanza wake ....funika wa kwako.....Inategemea ni kitu gani Mungu amekupa kuombea,...kama ni ofisi funika kazi maana huenda ukafukuzwa......Ukishasema unataka mabadiliko maana yake unataka kugusa kiti hivyo lazima ujipange vizuri3. Hakikisha unafanya toba kwa ajili ya jambo ambalo limesababisha kiti kikakufanyia fujo...Ufunuo 2:12...kwenye kanisa la Pergamo, Yesu hakufanya vita na shetani bali aliwaambia wa tubu......kiti ni matokeo ya kitu fulani...ni matokeo ya agano..ukiingia kwenye tuba unapata nafasi ya kuvunja uhalail wa kile kiti


4. Omba Mungu ahukumu juu ya miungu iliyosimamisha hicho kiti....Nitafanya hukumu juu ya miungu ya misri, in maana miungu ya misri ilihusika kwenye kiti cha enzi cha mzaliwa wa kwanza wa Farao.... kuhukumu ni kutenge kwa ajili ya kuadhibu...anaposeama omba Mungu aweke hukukmu inamaana hukumu ya Mungu ikate zile nguvu kutoka kwa mamdhabau...kiti hakina nguvu bila madhabau....ukisikia sheria haina meno maana yake hakuna nguvu ya kumbana mvunjaji.......Omba Mungu afanye hukumu juu ya hiko kiti maana kikitenganishwa na madhabau kina kosa nguvu ya kuendelea


5. HATUA YA TANO:
Sikia na fuata maelekezo binafsi unayotakiwa kuyafanya kwa kila kiti cha enzi kivyake...Ufunuo 3: 21-22 "Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi." na ufunuo 13: 2, 7 ....Vyote vinasema "mwenye masiko asikie".....


Mungu atakupa maelekezo binafsi, suluhisho la mapambano linaweza kuwa tofauti kwa kadri Roho atakavyokuelekeza.....Mifano michache: Math 2:13 " Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize."...kwa nini MUNGU hakupambana na herode badala yake akamwambia Yusuphu aondoke na mtoto......maelekezo ni muhimu sana.....mdo 12: 23... unakuta habari za herode mwingine na kanisa likaomba kwa juhudi kwa ajili ya Petro...ukiona ajenda ya maombi haijawekwa wazi kwenye biblia basi fuatlia majibu ya maombi....kanisa likaomba kwa juhudi lakina hatuambiwa liliomba nini...Ukishaona malaika peupe ujua kiti kiko kazini.....ukisahona malaika kaingia kazini ujue sio vita nyepesi....
Kuna ngazi fulani ya maombo kile kiti ulichoketi hakuna namna kinaweza acha kisiweze kuingia kazini....Baada ya herode kufa neno likakendelea...hawakuomba herode afe....Hata wakati wa Musa, musa hakuomba wazaliwa wa kwanza wafe ....Daniel 5: 17-21 " 17 Ndipo Danieli akajibu, akasema mbele ya mfalme; Zawadi zako zishike wewe mwenyewe; na thawabu zako mpe mtu mwingine; walakini nitamsomea mfalme maandiko haya, na kumjulisha tafsiri yake.

18 Kwa habari zako, Ee mfalme, Mungu Aliye juu alimpa Nebukadreza, baba yako, ufalme, na ukuu, na fahari, na utukufu;19 na kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa kabila zote, na mataifa, na lugha, wakatetemeka na kuogopa mbele yake; aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka kumwacha hai, alimwacha hai; aliyetaka kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka kumshusha, alimshusha.

20 Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, aliuzuliwa katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake.21 Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda-mwitu; akalishwa majani kama ng'ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote." note aliezuliwa yaani aliondololewa na kile kiti kikalindwa...kile kiti hakikuondolewa bali kililindwa....Nebukadreza aliinuliwa ili jeremia kama nabii akitoa adhabu nebukadreza aitekeleze....Nebukadreza alikosea kutengeneza sanamu wakati sanamu haikumpa kiti....Daniel 4: .....


Unatakiwa ucheki Mungu anasema nini juu ya hilo tatizo....


Kosa la nebukadreza ni karibu na la sulema na lakini adhabu tofauti......Kama kiti cha enzi kiko kanisani unafanya nini, Zabur 89:44 .."kiti chake cha enzi ukeitupa chini"...kwenye maombi unaweza kukitupa kile kiti cha enzi lakini si kila kiti cha enzi unaweza kitupa chini...maana unaweza kuta kiti ni cha Yesu amekiweka...hivyo unawajibika kushughulika na aliyeketi kwenye kiti.....Lazima ujue kiti kinaweza tupwa chini baada ya kushughulika na misingi yake na yale mambo manne tulijifunza hapo juu.....kiti cha shetani kanisani kinafuata nini?. ...aliyeketi ni mtumishi wa Mungu.....Mungu aliamua kwanza kudili na mtumishi wake.....akishatubu anarudi vipi kuketi kwenye kiti kile kile cha shetani?......anatakiwa abadilishe kiti ili asijerudia kutubu.....
Usiguse kiti kama hujaketi...Mithali 9:14..., Ayubu 29:7...njia kuu inawea kuwa na kiti na mahali pa mjini palipoinuka panaweza kuwa nakiti...unaweza kuelewa kwa nini ukiamka asubuhi kwenye njia unaweza kukuta sadaka....viti vyote vina mamlaka juu ya wanaoitumia njia...."Ezekieli 27:3 umwambie Tiro, Ewe ukaaye penye maingilio ya bahari, uliye mchuuzi wa watu wa kabila nyingi, mpaka visiwa vingi, Bwana MUNGU asema hivi; Wewe, Tiro, umesema, Mimi ni ukamilifu wa uzuri"....ilishiugulikiwa na viti vya enzi........Mithali 21:1..."Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa Bwana; Kama mifereji ya maji huugeuza po pote apendapo."...moyo wa kiongozi u mikononi mwake..maana yake Roho mtakatifu anaweza kukuletea kumbalisha moyo wa mtu kama ukikaa kwenye kiti,....Si kila mtu anaweza fanya hayo maombi, jaribu kuwa meneja wa kampuni hii na umfukuze meneja wa kampnuni nyingine uone kama utaweza....Inategema unaomba kutoka katika mamlaka yapi....Huwezi kupewa mamlaka juu ya viti/kit na ukawa na kiburi.....Kumbuka hufanyi kazi peke yako bali na kristo...na Roho mtakatifu atakuongoza...."Yohana 16:12 Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa."


MWISHO.
Ili kupata somo hili CD na DVD wasiliana na wahusika wa huduma ya MANA iliyochini ya mwalimu Christopher Mwakasege kupitia tovuti hii BONYEZA HAPA
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.