SOMO: WATU HAWASEMI, LAKINI WANAAMBIANA

Na Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.

Mara nyingi kwenye maisha yetu ya kila siku tumeona watu wanakuwa wanatunyamazia kwa namna moja au nyingine kuhusu swala/jambo fulani linalokuhusu wewe binafsi, ili hali wewe ukifikiri wako kimya, ukweli ni kwamba watu hawasemi tu lakini wanaambiana kuhusu wewe na kila jambo unalolifanya kwenye maisha yako ya kila siku. Mara nyingi kuna mambo mengi yanaweza kuwa yanajadiliwa kuhusu wewe lakini hauwezi jua maana hakuna anayekumbia.

Tambua kila unachofanya kwenye maisha yako ya kila siku watu wanaambiana hata kama kiwe kizuri au kibaya, kiwe cha kupendeza au cha kuchukiza lakini wataambiana tu.

Mara chache sana watu wanakaa kuzungumza habari za mafanikio ya mtu namna anavyopiga hatua kwenye maisha yake kwenye nyanja mbalimbali na kuweza kufanikiwa kiimani, kiuchumi, kisiasa na hata kijamii pia. Watu wengi wanapokaa pamoja mara nyingi huongea mambo ambayo saa nyingine yanaweza yasikufurahishe ukiyasikia lakini ndivyo watu walivyo. Ni ngumu kuyasikia maana hawatokwambia.

Hakikisha kila hatua na jambo unalolifanya innkuwa kwa usahihi na umakini mkubwa hata iwapo watu hawakuoni. Wanaweza kujifanya hawakuoni lakini kiukweli wanakutazama tu na wanangojea wakutane na watu wengine ambao wako kama wao ili waanze kuzungumza bila ya wewe kujua.

Uaminifu katika kufanya jambo fulani hautegemeani na watu wangapi wanakutazama au hawakutazami. Unaweza ukahisi hujaonekana kumbe uko wazi mbele ya macho ya watu. Hakikisha unafanya jambo kwa umakini na uaminifu mkubwa. Unapofanikiwa kufanya vizuri jambo fulani litaacha alama fulani kwenye maisha ya watu wengine. Mungu hutumia watu kukupandisha juu na hutumia watu kukushusha chini pia. Ni Muhimu kuhakikisha unakuwa makini. Watu hawasemi lakini wanaambiana.

Mwisho imekupasa kuwa makini namna unavyojiwakilisha mbele ya watu. Awe mtu wako wa karibu unayemwamini au usiyemwamini ni muhimu kuchukua tahadhari mapema. Fanya maswala yako kwa uaminifu kama ambavyo ungetamani wengine wakufanyie hata iwapo watu hawakuoni. Hakikisha haufanyi vitu kwa uzembe, fanya kwa umakini huenda wanajifanya hawakuoni lakini wanakuona. Fanya kwa kiwango cha juu lakini pale ambapo unaona umefika mwisho acha. Jitahidi kuweka juhudi kwenye kila jambo unalolifanya na kwa umakini mkubwa sana. Watu hawasemi lakini wanaambiaana.

E-mail:naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless Y’All
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.