SOMO: UHUSIANO WA VITI VYA ENZI NA MAFANIKIO YAKO (4 & 5) - MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE

Mwalimu Christopher Mwakasege

Karibu katika mwendelezo wa dondoo za somo la Uhusiano wa viti vya enzi na mafanikio yako kama lilivyofundishwa na mwalimu Christopher Mwakasege mapema mwezi March mwaka huu katika Viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam. Kama hukubahatika kusoma sehemu zilizopita basi BONYEZA HAPA. kama ulishasoma, endelea na somo hili hapa chini kwa sehemu ya 4 na 5. Barikiwa


UHUSIANO WA VITI VYA ENZI NA MAFANIKIO YAKOSiku ya 4

Ufunuo 13:2,7

Nini maana ya watakatifu

Watakatifu ni mtu aliyetengwa kwa kusudi maaalumu la Kimungu na si kila mkristo ni mtakatifu

Rum 8:31-39

Efeso 2:6

Efes 1:20

Ufunuo 3:14,21

Usijaribu kupambana na viti kabla hujaket katka kiti cha enzi


Swali:

{#}Utajuaje kama mafanikio yako yamekwamishwa na kiti cha enzi au viti vya enzi?

{#}Utajuaje kama unapambana na kiti cha enzi au wanadamu?


Kuna utofauti ya maneno na matendo yanayotoka katka kiti,unaweza ukakuta viongoz wanayoyaongea siyo wanayoyatenda

Shetani hutumia kiti cha enzi kma miongon mwa silaha yake kubwa sana

Ishara zinazokuonyesha kwamba unapambana na kiti cha enzi

1/:aliye katika nafasi ya kukupa haki yako anashindwa kukupa haki yako ukiona ivo unapambana na kiti

Mfano:

Mat 27:17-26

Matendo 25:1-12,26:30-32

2/:kulazimika kutii maagizo au mafundisho hata kama hukubaliani nayo


Mfano

Ufunuo 2:12-15

Ukiona watu wanamna hii ambao wanashika mafundisho ambayo kwa logic yakawaida hayakubalik na unajarib kumfundisha mtu wa namna iyo na haelewi ujue unapambana na kiti

3/:Kiongoz aliye juu yako kutumia nafasi ya uongoz alionao ili walio chini yake walazimike kuifuata imani yake

Mfano:

Daniel 3:1-7

4/:Kuwekewa kikao kwa shauri linaloweza kuamliwa na mtu mmoja

Mfano:

Matendo 6:7-15

Ukiona matatizo ya ndoa yametoka kweny kikao cha watu wawil ikaenda kweny kikao cha ndugu au familia ujue kuna kiti kinachopambana hapo mahali

5/:Ofisi kutumika kukunyanganya kilicho halali yako kisheria

Mfano

1falm 21:1-29

6/:Vifo vya watu vinapotokea vinapokosa kuwa na majib kisheria au kiuongoz katka eneo husika ujue unapambana na viti


Mfano

Mat 2:16,17


Mauaji ya watoto yaliyotokea wakati Yesu anazaliwa watoto wengi walikufa lakini sheria ilinyamaza na uongozi umenyamaza pia

Vivyo hivyo ilitokea wakati Musa anazaliwa


Antipasi aliuawa kanisan uongoz ulinyamaza na sheria ilinyamaza hakuna kilichoongelewa


SOMO: MAHUSIANO YA VITI VYA ENZI NA MAFANIKIO YAKO

MSEMAJI: MWL. C. MWAKASEGE

SIKU YA TANO:


Ufunuo 13:2,7

Mathayo 23:1-3

Shetani anawapa watu wake nguvu, kiti cha enzi, na uweza mwingi.

Lengo ni kufanya vita na watakatifu na kuwashinda.

Shetani ameachilia viti vyake katika ngazi mbalimbali kama kanisani, kabila, ukoo, taifa, lugha, nk

Jana nilikuonesha ishara zinazoonesha kwamba vita uliyonayo unapambana na viti vya enzi. Leo tuendelee mbele zaidi:

7. Unapoona ofisi za viongozi wa dini na viongozi wa dola wanapoungana pamoja ili kupinga kile kizuri unachoifanyia jamii

Matendo 3:

Matendo 4:

Utaona hapa akina petro wanawekwa gerezani baada ya kumponya kiwete na kuhubiri injili watu kuamini.

Utaona viongozi wa dini na dola kwa pamoja wanawauliza akina petro ni nguvu gani na kwa jina gani mmetenda haya?

Hawana shida na mtu kupona, shida yao ni mamlaka ipi wametumia?

Ukiona hivyo ujue hiyo vita inatoka kwenye kiti cha cha enzi kilichowekwa na shetani.


8. Unapoona kiti kishindwacho katika vita ya viti vya enzi katika ulimwengu wa roho watu wake wanakuwa na hasira isiyo ya kibinadamu na haina maelezo kiutu.

Ufunuo 16:10,11

Tunaona malaika anapeleka adhabu kwenye kiti, na ufalme wote unatiwa giza na watu waliotumika katika hicho kiti wanapata maumivu, na hasira.

Pia wanatukana. Ukiona hivyo ujue hiyo vita ilikuwa ni ya viti.

Mfano: mkoa mmoja pepo mmoja lilikutana na nguvu za Mungu likaanza kuachilia matusi, tukajua kwamba kiti chao kimepigwa na kiti tulichokalia katika Yesu.

9. Kuoteshwa ndoto au kuoneshwa maono yanayozungumzia juu ya kiti cha enzi na mafanikio yako

Daniel 4:1-15

Daniel 5:17-21

Nebukdreza aliota ndoto

Ayubu 29:7,19,25

Mara ingine utaona kiti au kisiki katika ndoto. Utajua kwamba hiyo vita uliyonayo inatoka katika viti vya enzi.

Soma hiyo mistari ya ayubu utaelewa vizuri

10. Kuwekewa vikwazo kikazi vinavyokulenga wewe bila kuonesha wazi kwamba vinakulenga wewe ili tu uache kazi

Daniel 6:1-17

Hapa watakupambanishi na kiti kilichokupa kiti.

Haleluya! Unasema mwakasege unaongea kiti gani? Soma biblia yako.

11. Tazama mazingira ambayo Mungu amekupa uishi na utumie kupata kipato, kuna nini?

Penye utawala wa kiti huwa kuna alama ya kiti.

Waamuzi 6:25,26,28,30

Kulikuwa na madhabahu na ashera. Gideoni aliharibu madhabahu na kuikata ashera. Alipofanya hivyo watu wa mji walichukia kwa sababu ile viti ilikuwa ni ya viti.

Madhabahu peke yake bila kiti haina mamlaka ya kutawala kisheria

Madhabahu inatumia kiti kutawala

Kiti kinatumia nguvu za madhabahu kutawala

Madhabahu na kiti vinatakiwa kufanya kazi pamoja.

Unaweza kubaki na madhabahu na kiti umekabidhi kwa Mungu mwingine.

Mfano:

Nilienda nchi mmoja ulaya. Nilipata nafasi ya kutembelea kanisa fulani. Kwenye eneo la kanisa nikakuta mti umesimamishwa na juu umewekwa vitu kama masikio. Wenyeji waliniambia wao wanatoa msaada kwa wahindi wekundu, kwa hiyo hao wahindi wakawapa zawadi ya Mungu wao kama shukrani ya misaada wanayopokea.

Unaona wana madhabahu, lakini kiti wamekabidhi kwa Mungu mwingine. Angalia kiroho chao kilianza kuharibika.

Vita ya viti ni ngumu sana. Kuna mtu mmoja Ethiopia aliona watu wakiabudu kwenye mti siku nyingi, alivyoonakufariki hvyo alichukua shoka kwenda kukata. Mti ulivyoanguka naye akaanguka na hapohapo.

Kwanini? Yeye alienda na shoka kumbe wao wameenda na viti.

Ooh! Hii ni siri ya ajabu unahitaji kufahamu. Nilikwambia sikutaka kufundisha hili somo, lakini Mungu akanibana nifundishe.

Masomo kama saa ingine hatufundishi watu wote, unachukua wachache unasema nao. Maana ni mazito

Lakini ukiona Mungu ameachilia wazi namna hii ujue kuna mahali anatupeleka ni kuzuri sana.

Kesho nitakufundisha namna ya kuangalia kama umekaa kwenye kiti au hujakaa.

Somo litaendelea wiki ijayo.. Barikiwa

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.